Tamko la BAVICHA mkoa wa Arusha kumlaani Tendwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la BAVICHA mkoa wa Arusha kumlaani Tendwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwan mpambanaji, Mar 17, 2011.

 1. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Baraza la vijana mkoa wa Arusha (BAVICHA)
  Tel 0784 834152
  bavichaarusha@gmail.com  TAMKO LA BAVICHA KULAANI MATUMIZI MABAYA YA OFISI YA MSAJILI

  Ndugu wanahabari,

  Katika siku za karibuni msajili wa vyama vya siasa ndugu John Tendwa ametoa kauli mbalimbali zenye kuashiria kukipendelea chama cha ccm na serikali yake.

  Mtakumbuka kuwa Twenda alitishia kukifuta Chadema kwa madai ya kuchochea vurugu katika maandamano yake, kimsingi sisi BAVICHA mkoa wa Arusha tunapinga kwa nguvu zote kitendo hiki cha msajili wa vyama kukipiga mkwara CHADEMA,Tendwa alipaswa kwanza kuiandikia barua CHADEMA kabla ya kuipiga mkwara, kwa kitendo chake cha kutoa kauli hii ni dhahiri kuwa nia yake ni kukifuta chadema kwa madai yasiyokuwa na msingi wowote wa kisheria, tunalaani kauli hii na haya ni matumizi mabaya ya ofisi ya umma ambayo inalipiwa kwa kodi za wananchi wote.

  John Tendwa kwa kuwa wewe ni mwanasheria tena jaji mstaafu ni dhahiri unajua sheria,hivyo tunahoji unawezaje kutoa hukumu bila kusikiliza upande wa pili?Ni wakati gani,wapi viongozi wa CHADEMA walitumia lugha ya kuvuruga au kuchochea chuki? Toa ushahidi wa haya unayotuhumu chadema vinginevyo tutaamini kuwa umetumwa na unatumika.Ni ukweli kuwa sukari, mafuta na gharama nyingine za maisha zimepanda na ambacho CHADEMA tumefanya ndio wajibu wetu kama chama cha siasa
  Lakini pia tunalaani majibu yako ya kiwendawazimu kwa katibu mkuu wetu Dr Slaa, umenukuliwa ukidai kuwa yaliyotokea Arusha ni sahihi. Je barua yako yenye kumb ……………………..ya kuruhusu maandamano ya CHADEMA pamoja na mkutano ilikuwa batili? Je nani anakupa mamlaka ya kuzungumzia tukio la Arusha wakati lipo mahakamni?

  Je wewe ni nani hata useme Dr slaa aliharibu kwa Mungu sembuse kwa binadamu?hatukubaliani na wewe kuwa Dr Slaa ana ufinyu wa kufikiri,tunakutaka umwombe radhi.

  Bavicha mkoa wa Arusha tunamtaka Tendwa aache kutoa kauli za vitisho maana hizi ndio zinachochea chuki, na ni hatari kwa usalama wa taifa, na kamwe hawezi kukifuta CHADEMA tutakilinda chama chetu, tutakitetea kwa nguvu zote. Hatuandamani kwa ajili ya pesa au uchu wa madaraka,tupo hapa kupigania haki na ustawi wa taifa letu na tuko tayari kwa lolote.

  Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu na CHADEMA ni sauti ya watanzania wote, ni sauti ya ukombozi wa kweli wa taifa.

  NANYARO E.J.
  Mwenyekiti BAVICHA (M)

  BAVICHA Arusha (M)
  +255 784 834152
   
 2. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Bhita ni bhita haina masho
   
 3. s

  smz JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tendwa, kama mlivyosema ni mwanasheria na anajua kuwa anafanya kinyume, na hii yote ni njaa, anatetea kitumbua chake.
   
 4. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tendwa ni kama msukule,hajui afanyalo wala atendalo,na hajui mipaka ya kazi yake,Maandano ya Cdm yanahatarisha amani yake na wenzake ya kuiba mali ya tz bla kukamatwa,KAMA CDM BAVICHA MBEYA,tunaungana nanyi wa A-town kulaani kauli ya Tendwa
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Mambo yanogile Bavicha na muendelee hivyohivyo vijana ndio walinzi wa nchi hii mukiachia kikundi kidogo cha mafisadi na vitoto vya mafisadi na mapandikizi kama akina Tendwa nchi haitasonga mbele kama Jaji alikosea kuegemea upanda mmoja,hakikisheni munasimama imara kulinda rasirimali za taifa kwa manufaa ya kizazi kijacho cha watanzania,Tafadhali mungempa dose Sophia Simba na Wasirra pia
   
Loading...