Tamko la BAVICHA mkoa wa Arusha kuipongeza kamati kuu ya CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la BAVICHA mkoa wa Arusha kuipongeza kamati kuu ya CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwan mpambanaji, Apr 2, 2011.

 1. M

  Mwan mpambanaji JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2011
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 468
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  BARAZA LA VIJANA CHADEMA MKOA WA ARUSHA(BAVICHA)
  P.0.BOX 12525
  ARUSHA
  TEL.0754 834152
  Email.arushabavicha@gmail.com
  Tovuti ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)


  TAMKO LA BAVICHA MKOA WA ARUSHA.KUIPONGEZA KAMATI KUU YA CHADEMA PAMOJA NA KUUNGA MKONO SIKU 21 ZA SERIKALI KUTATUA SWALA LA UMEYA WA ARUSHA

  Ndugu wanahabari
  Mtakumbuka kuwa kamati kuu ya Chadema iliketi tarehe 19.3.2011,pamoja na maazimio mengine,ilitoa siku 21 kwa serikali kutumia busara kutatua swala la umeya wa Arusha,ambao sote ni mashahidi ya jinsi ulivyokiuka sheria.Bavicha mkoa wa Arusha tunaipongeza kamati kuu,kwa jinsi ambavyo wamekuwa na busara na jitihada zote za viongozi wetu kuzuia umma wa Arusha.Ni busara za viongozi wetu ambazo zimefanya hadi sasa umma wa Arusha umekuwa na subira,tukiamini kuwa kama serikali itatumia busara basi swala la umeya litatatuliwa kidiplomasia,siku 21 zinatosha kabisa kwa serikali kama ina nia ya kweli na dhamira zao zinawatuma hivyo
  Bavicha mkoa wa Arusha,tunapenda kuihakikishia kamati kuu na umma wa Tanzania kwa ujumla kuwa,tupo imara,na tupo tayari kupambana hadi ushindi upatikane,vijana na umma wa Arusha hatutakubali wala kuendelea kuvumilia ukiukwaji huu wa sheria katika uchaguzi wa meya,na kamwe hatumtambui wala hatutamtambua meya ambaye si chaguo la wanaarushaNi lazima uchaguzi urudiwe ili haki itendeke,maana msingi wa maendeleo ni HAKI,na bila haki hamna maendeleo wala Amani.Tunasisitiza kuwa baada ya siku 21 tutaingia mitaani kushinikiza uchaguzi wa meya,vijana tupo tayari kwa mapambano,hatutaogopa wala kutishwa na awaye yote,tutapambana hadi kieleweke.

  Ikiwa hakuna jambo lolote muhimu ambalo mtu yupo tayari kufa kwalo,basi mtu huyo hastahili kuishi,Martin Luther King Jr


  NANYARO E.J.
  MWENYEKITI BAVICHA (M)
  ………………………………..
   
 2. utemi

  utemi Senior Member

  #2
  Apr 2, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 167
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
 3. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Duh,kuna kupumua kweli mwaka huu?
  Hata babu saivi hampumzishi tena JK
   
 4. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #4
  Apr 2, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0


  Duh kweli nimeamni chadema mna uchu wa madarak mnataka kumwaga damu tena Arusha! Hivi kama sheria imepindishwa kwa nini msiende mahakamani! Katika wale waliokufa kuna Bavicha hata mmoja alikufa!? Au safari hii mnataka Bavicha mmoja aondoke? Nashauri njia ya mahakama itumike!
   
 5. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
 6. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #6
  Apr 2, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mzito Kabwla,

  Hivi kweli unafikiria kutumia nini? Just think ni lini wameanza kupata hiz mil 200? nini manufaa ya kununulia kila mwenye wajibu laptop? Naamini tutafika tu huko. what can you do? Just help them. Naomba tafadhali na wewe usiwe unaipinga CCM ilahali unaiunga mkono bila kujijua.

  asante
   
 7. m

  mareche JF-Expert Member

  #7
  Apr 2, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 475
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  cdm uyeeeeeeeeeeeeeeeeeeee naunga mkono hoja
   
 8. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #8
  Apr 2, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Mzito kabwela,sijui kwa dunia ya leo ulitaka tutumie njia gani ya mawasiliano zaidi ya mobile,email yetu ni arushabavicha@gmail.com,je hata gmail ni ya vichoChoroni?
  Sisi bavicha arusha tumejipanga na kamwe hatuwezi kukubali sheria zivunjwe kwa sababu yoyote ile,tutapambana hadi kieleweke
   
 9. lynxeffect22

  lynxeffect22 JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 625
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hii imetulia! ... mpaka kieleweke
   
 10. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  naona kama vijana wametumia lugha kali!!!
   
 11. Mbaneingoma Zom

  Mbaneingoma Zom JF-Expert Member

  #11
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapo BAVICHA mmenena kwani tulisubiri sana muongozo wa namana ya kudai haki yetu ila tumeshapata kwamba tutavumialia mpaka hizo siku ishirini na moja zipite baada ya hapo sote tutaungana na ninyi kwenye suala zima la kudaai haki!!
   
 12. Mbaneingoma Zom

  Mbaneingoma Zom JF-Expert Member

  #12
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 201
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe unakiherehere kama jina lako lugha kali hapo iliyotumika ni ipi? Unajua maana ya lugha kali au unajifunza kiswahili ebu tupishe kule.
   
Loading...