Tamko Kutoka Jukwaa la Wakristo Kuhusu Zanzibar

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) limetoa tamko kuhusiana na hali ilivyo sasa Zanzibar likisema linafadhaishwa na kusikitishwa nayo na kwamba linaamini isingefikia hapo endapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingechukua hatua katika kutatua mgogoro huo.

Katika tamko hilo lililosambazwa kwenye vyombo vya habari jana baada ya kikao cha TCF juzi, yamo mapendekezo manne likiwamo la kuitaka Serikali kurejesha mchakato wa Katiba kwa kuzingatia maudhui yaliyomo katika Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ili kuondoa utata wa Serikali kushiriki masuala ya Zanzibar.

“Sisi viongozi wa dini tuliokutana leo tarehe 15.03.2016, tunafadhaishwa na kusikitishwa na hali ya Zanzibar kwa sasa.

"Hali ya Zanzibar isingefika hapo ilipo iwapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingechukua hatua ya kutatua mgogoro huu.

"Hali hii ya Zanzibar na udhaifu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano vinapelekea kushindwa kwa Serikali ya Muungano kuchukua hatua ya kusaidia hali ya Zanzibar. Hata hivyo, udhaifu huu wa Katiba hauondoi wajibu wa Serikali ya Muungano kuhakikisha haki na amani vinatawala Zanzibar,” ilisema sehemu ta tamko hilo lililotiwa saini na Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mwanza, Jude Ruwa’ichi.

Jukwaa halikufafanua hali ya Zanzibar kwa sasa inay- osababisha maaskofu hao kufadhaika lakini huenda limekusudia kueleza hofu iliyotanda katika visiwa hivyo tangu Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ilipofuta uchaguzi na matokeo yote ya uchaguzi wa Zanzibar, na baadaye kutangaza kuwa utarudiwa Machi 20.

Vyama tisa kikiwamo Chama cha Wananchi (CUF) vilitangaza kujitoa lakini ZEC imesisitiza vyama vyote vitashiriki.

Hali imeendelea kuwa tete na hivi karibuni yamekuwapo matukio ya uchomaji moto makazi ya watu katika visiwa hivyo yanayoonyesha uvunjifu wa amani kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa marudio Jumapili ijayo.

Baadhi ya matukio hayo ni kuchomwa moto maskani za CCM na CUF, nyumba 11 za watu ikiwamo ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame iliyoko Kijichi, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Baada ya kutathimini hali hiyo, TCF imesema pamoja na udhaifu wa Katiba, Serikali ya Muungano bado ina wajibu wa kuhakikisha uhuru, haki na amani vinatawala Zanzibar kuelekea uchaguzi huo wa marudio.

“Hata hivyo, Serikali ya Muungano pamoja na taasisi zinazosimamia mchakato wa uchaguzi, zinao wajibu wa kuhakikisha kuwa suala la uhuru, haki na amani Zanzibar vinalindwa na kuheshimiwa. Suala la uhuru, haki ni wajibu wetu sisi viongozi wa dini na Watanzania wote na halina mbadala,” ilisema sehemu ya tamko hilo.

Jukwaa limesisitiza kwamba ni jukumu la kila mmoja kutimiza wajibu wake kulinda uhuru, haki na amani na kuweka uzalendo kwanza kuliko kutanguliza maslahi binafsi au ya vyama vya siasa.

Mbali ya pendekezo la kuitaka Serikali kurejesha mchakato wa Katiba, pia limewataka viongozi wa dini kuwahimiza Watanzania wote kuendelea kuiombea Tanzania (Bara na Zanzibar) ibaki kuwa Taifa lililojengwa katika msingi ya uhuru, haki na amani.

Pili, limelitaka Jeshi la Polisi, vikosi vya ulinzi na usalama na Jeshi la Wananchi wa Tanzania, kwa wakati huu kuendelea kutimiza wajibu wa kusimamia amani na taratibu kwa haki bila upendeleo.

Mwisho limesisitiza kwamba viongozi wa dini wabaki kuwa sauti ya kinabii na wahubiri wa uhuru, haki na amani wakati huu, wakati wa uchaguzi na haada ya uchaguzi.

Chanzo: Mwananchi
 
"Hali ya Zanzibar isingefika hapo ilipo iwapo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingechukua hatua ya kutatua mgogoro huu.

Hawa viongozi walikuwa wanatakiwa kwanza wasome katiba ya muungano,katiba ya zanzibar na Sheria ya uchaguzi ya Zanzibar kabla ya kutoa tamko lao.Uelewa wao wa hayo maeneo matatu ni mdogo mno,

Katiba ya muungano inaeleza wazi wazi mambo ya muungano ni yepi.Uchaguzi wa Zanzibar si swala la muungano.Serikali ya muungano inashughulikia mambo ya muungano tu yaliyoko kwenye katiba.

Katiba ya Zanzibar inatamka wazi kuwa Zanzibar ni nchi kamili.Raisi wa muungano hata akienda kule huenda kwa kualikwa na raisi wa Zanzibar hawezi kwenda tu kama afanyavyo bara kwenda mkoa wowote.

Sheria ya uchaguzi ya Zanzibar inatamka wazi kuwa tume ya uchaguzi ya nchi ya Zanzibar (ZEC) ni tume huru ambayo haiwezi ingiliwa na yeyote awe raisi wa Zanzibar au muungano au yeyote.

Kama ni katiba inayotakiwa ibadilishwe ni katiba ya Zanzibar iruhusu Raisi wa muungano kuingilia kati.Lakini hawa viongozi wa Jukwaa la wakristo wanaonyesha kuwa wao ni UKAWA wanaongea kubadilisha ya muungano! Katiba ya muungano ikibadilishwa isipobadilishwa ya Zanzibar ni kazi bure.
 
Lakini bwana Load alikimbia kule znz kusimamisha nini tena vile
 
Wanachosema kina mantiki sana ila unafiki wao unatokana na wao kuchelewa kuyazungumza hayo mpaka imebaki siku 4 tu ndio wanazungumza? Tunajuaje walisetiwa ili wazungumze hivi juzi?

HAPO NDIPO PIA NAKUBALI KUWA NI WANAFIKI.
 
Nilishangaa sana juzi BAKWATA kuunga mkono serikali na uchaguzi wake wa marudio.
Wakati wanaoteseka na seke seke la Zenji ni waumini wao
 
Hawa viongozi walikuwa wanatakiwa kwanza wasome katiba ya muungano,katiba ya zanzibar na Sheria ya uchaguzi ya Zanzibar kabla ya kutoa tamko lao.Uelewa wao wa hayo maeneo matatu ni mdogo mno,

Katiba ya muungano inaeleza wazi wazi mambo ya muungano ni yepi.Uchaguzi wa Zanzibar si swala la muungano.Serikali ya muungano inashughulikia mambo ya muungano tu yaliyoko kwenye katiba.

Katiba ya Zanzibar inatamka wazi kuwa Zanzibar ni nchi kamili.Raisi wa muungano hata akienda kule huenda kwa kualikwa na raisi wa Zanzibar hawezi kwenda tu kama afanyavyo bara kwenda mkoa wowote.

Sheria ya uchaguzi ya Zanzibar inatamka wazi kuwa tume ya uchaguzi ya nchi ya Zanzibar (ZEC) ni tume huru ambayo haiwezi ingiliwa na yeyote awe raisi wa Zanzibar au muungano au yeyote.

Kama ni katiba inayotakiwa ibadilishwe ni katiba ya Zanzibar iruhusu Raisi wa muungano kuingilia kati.Lakini hawa viongozi wa Jukwaa la wakristo wanaonyesha kuwa wao ni UKAWA wanaongea kubadilisha ya muungano! Katiba ya muungano ikibadilishwa isipobadilishwa ya Zanzibar ni kazi bure.
Usidanganye watu, kitu gani huru. Tumenyamaza na kufunika kombe kumpisha mwanaharamu apite. Ikiwa huru nani alikwenda kumshusha kwenye kiriri huku akiendelea kutoa matangazo ya matokeo na kumpeleka makao makuu Naibu mwenyekiti wa Tume. Wapi Jech kalitolea tangazo la kufutwa uchaguzi na kitu gani kilichomfanya awaache makishna wenzake Bwawani hku akitoa tngazo la kufuta uchaguzi kutoka studio zisizoeleweka. Huo ndio uhuru wa tume.
 
Wanachosema kina mantiki sana ila unafiki wao unatokana na wao kuchelewa kuyazungumza hayo mpaka imebaki siku 4 tu ndio wanazungumza? Tunajuaje walisetiwa ili wazungumze hivi juzi?

HAPO NDIPO PIA NAKUBALI KUWA NI WANAFIKI.
Ccm ni janga kuu Tanzania
 
Hawa jamaa kutiwa acid kote bado wako na kujipendekeza tu na Wazanzibari.
 
Wameweza kuzungumza pasipo kujipendekeza. Kuna wengne wanakuwa na woga. But mapema tu nakumbuka walisema suala hili maaskof pasipo kujiuma uma. Na wamejarib siku zote kuwa neutral.

Wanachosema kina mantiki sana ila unafiki wao unatokana na wao kuchelewa kuyazungumza hayo mpaka imebaki siku 4 tu ndio wanazungumza? Tunajuaje walisetiwa ili wazungumze hivi juzi?

HAPO NDIPO PIA NAKUBALI KUWA NI WANAFIKI.
 
Kama hivi ndivyo, CCM hii hii na serikali yake ilitumia katiba gani mwaka 1984 kumfukuza Aboud Jumbe Mwinyi kutoka nafasi ya urais akiwa amechaguliwa na wananchi wa Zanzibar lakini leo CCM hiyo hiyo na serikali yake ishindwe kuchukuwa hatua?
Hapa kuna mambo tunadanganyana ama yanafichwa.
 
Ni kichaa tu anayeweza kuona jambo la Zanzibar kama utani fulani hivi ,Japo Bakwata wao wameunga mkono uchaguzi wa marudio
BAKWATA hata wakisikia wazanzibar woote wamekufa hawatajali kabsa , hawasonononeshwi na chochote kile .
 
Back
Top Bottom