Tamisemi wametoa majina ya watoto walio dahiliwa kidato cha tano na vyuo mbalimbali. Majina yako kwa PDF lakini hayapo katika mpangilio na hauwezi kutafuta jina mojamoja kurasa ziko 5934 sasa uanze kusoma jina moja moja ukisaka jina la mwanao ni changamoto kidogo. Isitoshe website inafunguka kwa mbinde na MB zinaliwa ka nini, hebu tusaidieni mutuwekee katika format rafiki. au miyapange majina kutumia namba za usaili au shule wanazotoka au wilaya wanazotoka kuliko ilivyo sasa katika mpangilio mbovu na usio eleweka.