TAMISEMI mulikeni ujenzi wa madarasa Tarime

TAMISEMI mulikeni ujenzi wa madarasa Tarime

Boko halal

Senior Member
Joined
May 14, 2014
Posts
175
Reaction score
124
Halmashauri ya wilaya ya Tarime ilipokea pesa za ujenzi wa madarasa sawa na halmashauri zingine nchi nzima lakini mpaka sasa ujenzi huu upo chini na unasuasua sana, maeneo mengi ujenzi upo hatua ya maboma huku madarasa machache yakiwa kwenye hatua ya upauaji.

Hatua hii ya ujenzi kusuasua inatia wasiwasi huenda ifikapo tarehe 17 January shule zikifunguliwa madarasa haya yatakuwa bado hayakamilika hivyo kupelekea kuwalazimu walimu kuwarundika wanafunzi darasa moja ambayo itakuwa hatari kwa afya zao.

Sababu kubwa inayofanya ujenzi wa madarasa haya kusuasua ni pamoja na kutumia wakandarasi baadala ya force accounts, mathalani Kuna Mkandarasi mmoja alipewa madarasa 60 (TAKUKURU imulike hapa huenda rushwa ilitumika) huku wakandarasi wengi wakiwa hawana uwezo wa kusupply vifaa vya ujenzi kwenye sites zao.

Kitendo cha kuwatumia wakandarasi kimefanya madarasa haya kujengwa chini ya kiwango kwa lengo la kubana matumizi na kutengeneza faida.

Tamisemi tumeni timu ya watalaamu Tarime ikague ujenzi huu pamoja na kujiridhisha na ubora vinginevyo tutakuwa na magofu na sio madarasa baada ya muda mfupi.

Tamisemi pia inapaswa kutoa muongozo ili kukwamua ujenzi wa madarasa haya ili shule zitakapofunguliwa madarasa haya yawe tayari kutumika.
 
Utaratibu wa force account unapingwa sana na chadema
 
Back
Top Bottom