TAMISEMI mnapotangaza "Form 5 selection 2023" mhakikishe yako mtandaoni tayari

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Nov 30, 2022
607
553
Habari,

Kumekuwa na tabia ya kipuuzi kwa baadhi ya vionhozi wa taasisi za serikali kutangaza matukio fulani na kusema yako mtandaoni tayari na kutoa muda wa ukomo wake wakati siyo kweli kuwa yako mtandaoni.

Jana tamisemi wametangaza kuwa selection za F5 ziko tayari na wakatoa muda wa siku 21 kwa wanaotaka kubadilisha kombi lakini ukiingia kwenye website yao majina hayo hamna.

Viongozi wa nchi hii mnapotoa matangazo yenu yaendane na uhalisia siyo mihemko,wekeni hizo selection watu waangalia na iwe kweli siyi siasa.

Kichwa cha habari kinasoma""CLICK HETE FOR TAMISEMI FORM FIVE SELECTION 2023" ukiingia ndani unakuta "First,Second,Third Selection, 2022"" kama siyo ujinga ni nini?
 
Back
Top Bottom