TAMISEMI bado zoezi la uhakiki linaenelea?

TAMISEMI bado zoezi la uhakiki linaenelea?

Sasunimg

Member
Joined
Aug 3, 2016
Posts
58
Reaction score
34
Jamani waungwana ivi uhakiki bado unaendelea?maana watu tumesubiri vibali vya uhamisho mpaka tumepoteza matumaini
 
we acha tu mkuu wangu,, watu tumesubili mpaka tumechoka.. mbaya zaida hata hao tamisemi hawasemi chochote!! kazi kweli
 
Uhakiki kwa sasa ni zoezi la kudumu, kuna watu wanastaafu, wanafariki, wanaacha kazi.Ila Kuna fununu kutoa chanzo kisicho rasmi kuwa mwezi February mambo yatafunguka.
 
Nasikia maticha wameambiwa wapeleke vyeti vya chekechea vihakikiwe na yeyote ambaye hakusoma ni bora ajiondoe mwenyewe kazini.
 
Wanahitaji zaidi cheti cha primary na cha 'O' level kwa sababu ndicho kilichozalisha vyeti vingine.
 
Wanahakiki kibubu chao, mpaka sasa hawaamini kama kipo empty.
 
Hivi wamewalipa watumishi malimbikizo yao?
Jibu ni hapana, masikini watanzania.
 
Kuhusu suala hili tunaomba Mbunge yoyote anayesoma hapa tunaomba jamani mtusaidie, yaani kazi ya serikali imekuwa kama kazi ya kwa Mhindi kweli, tunaomba kina Zitto , Bashe, kina Nape tunaomba tusaidieni sisi wafanyakazi tunaonewa ! tunaomba suala hili mtutetee bungeni. ukiangalira mfano hata sasa watu wanaotakiwa kupanda mwaka huu kimya, hatujui nini kinaendelea !

kitu kinachotushangaza ni kwamba ; watu wote walioteuliwa wamepewa mishahara mipya

1. mawaziri walioteuliwa akiwemo Kairuki mbona wamebadilishiwa mishahara
2. wakuu wa mikoa na wailaya walioteuliwa mbona wamebadilishiwa mishahara
3. ma RAS na maDAS wapya mbona wambebadilishiwa mishahara
ma
4. makatibu wakuu wa wizara mbona wamebadilishiwa mishahara n.k

kwanini watu waliotajwa hapo juu wasisubiri UHAKIKI ?
Kwanini ni watu wa chini tu ndo tunasubiri uhakiki wakati nyinyi wakubwa mnabadilishiana mishahara bila kusubiri uhakiki ?
 
Nikioa mke wa pili au wife akibebwa out nawalaumu hawa jamaa kwa kusitisha uhamisho na ndoa zetu zinaingia matatani....nashangaa kimya kimya...MBONA WAO WANAHAMA NAO.Au ndo mlolongo wa maisha ya MASHETANI yenyewe.!?
 
Alieshiba hamjui mwenye njaa, sio uhamisho tu na kupanda madaraja,

Kuna watu wamesitishiwa ajira June lakn kimya mpaka leo, HAKUNA jipya wala hakna taarfa zozote zile!

Wanaishi kishetani tu mtaani! AJIRA Mpya nazo kimya graduate wengne mwaka 2 wapo mtaani tu, lakn serikali inajfanya haijui kuwa watu wanahangaika!

MATAMKO NDO YAMETAWALA NA MAKANUSHO YASIYOISHA!
 
Kwa kuwa Watumishi ni Wapuuzi na wakuu wanajua kuwa ni wapuuzi, watu wakuitikia Kila Upuuzi kutoka Juu ndio mana yanatendeka hayo Yote.

Endeleeni kulia lia humu muone kama italeta Tija Yoyote. Tokeni Nyuma Ya Key boards Nendeni Mkaji organize kudai haki zenu.
 
Uhakiki kwa sasa ni zoezi la kudumu, kuna watu wanastaafu, wanafariki, wanaacha kazi.Ila Kuna fununu kutoa chanzo kisicho rasmi kuwa mwezi February mambo yatafunguka.
Hivi mtu mzima uliye na akili timamu unaishi kwa kutegemea "tetesi"???

Kwanini haiwekwi Wazi?
 
Back
Top Bottom