1)Kifo ni haki yetu,wote kitatuchukua Hakuna myongoni mwetu,kitakae mbakiza Kifo ni kivuli chetu,nasi kipo twatembe Pumzika kwa amani,Richad Tambwe wa Hiza.
2)Mauti ndie mlangio,nawe umeshaingia Mauti kama mchango.sote tutauchangia Mauti hayana hongo,eti tukayakimbia Pumzika kwa amani,Richad Tambwe wa Hiza.
3)Tambwe umetangulia,na sisi tunafwatia Chadema ya kulilia,na yako famili pia Kifo ndio yetu njia,sote tutakipitia Pumzika kwa amani,Richad Tambwe wa Hiza.
4)Tambwe mwana harakati,nchi kuipigania Kasi kusini na kati,kule ulifikiria Na kupanga mikakati,maendeleo Pumzika kwa amani,Richad Tambwe wa Hiza.
5)Kwa moyo kwa kijasiri,gari ulijiwashia Hukujua ya kujiri,kifo cha kukaribia Hakika kumbe tayari,saa imeshafikia Pumzika kwa amani,Richad Tambwe wa Hiza.
6)Kazi yako duniani,tayari imetimia Twakombea kwa manani,pema kupumzikia Fikra zako jukwaani,sote tutazienzia Pumzika kwa amani,Richad Tambwe wa Hiza.