Deejay eXii
Member
- Feb 22, 2025
- 40
- 44
THE TOMORROW WAR (2021)
_______
Genre: Sci-Fi, Action, Thriller
Duration: 138 minutes
Rating: 6.6/10 (IMDb)
Origin: USA
Director: Chris McKay
_______
SHORT STORY BEHIND
Ujumbe wa dharua unaifikia Marekani Miami, Florida. Ujumbe unasema,"We are you. 30 years from now We are fighting a war 30 years in the future. The human race is losing. We need you to fight for our survival.", Mwanamama huyo Jenerali anaongeza kwa kusema,"If you think we’re here to ask you to do something for us, you’re wrong. We’re here to ask you to fight. For your lives, for your future."( Yai lipo huko kweli au mpaka nitafsiri tena...!?😂😂)
Maneno haya yalikuwa hatua muhimu ya kuzindua harakati za kijeshi na kutangaza dharura kwa jamii ya sasa ili kushirikiana na vikosi vya kijeshi vilivyosalia kupambana dhidi ya tishio la miaka 30 mbele. Jenerali Sherman, alilazimika kutoa taarifa ya dharura kwa jamii ili kuwaomba msaada kutoka kwa kizazi cha sasa, ambapo watu walilazimika kujiunga na vita hivyo ili kuokoa dunia.
Dan Forster, Mme, Baba na mhadhiri Katika chuo kikuu ndani ya mjii wa Florida. Former US Marines Force anajikuta katika shinikizo la kujumuika kujitolea kwenda vitani. Kwa pamoja familia ikagawanyika Mke(Maggie) na bintiye(violent) wakiamini kujitolea kwake kunaweza kuwa mwanzo wa wao kubaki bila Dan. Hakuna namna maana kama una mapenzi ya kweli na familia yako utafanya kila kitu kuilinda. Forster anaungana na vikundi vingine vya watu wanaokubali kwenda katika future kukabiliana na jinamizi wasilolijua ambalo hata serikali ilishindwa kuliweka wazi kulinda taharuki na woga kwa wananchi wao.
Uenda magonjwa mengi yako mbele ya muda wetu kama ilivyokuwa Corona na kama tungeweza tungewai kuzuia kabla ya yale yaliyotokea. Ila sasa 'White Spikes' ni janga lingine linalotakiwa kushughulikiwa kwa haraka sana. Kama white spikes wakifaniki kudominate maana yake itachukua miezi michache sana wao kutoka 2051, kuja kuangamiza ulimwengu wote wa miaka hii.
Safari ya kwenda katika future inaanza na hitilafu katika mtambo wa kusafirisha unasababisha landing mbaya kwa raia wote wengine wakiangukia katika vyuma na sehemu ngumu na kusababisha kupoteza maisha hata kabla ya operation dhidi ya White Spikes. Dan Forster na rafikiye wa muda mfupi wanafanikiwa kudondokea katika swimming pool na kuwa salama yao. Wakiwa na maraia wengine kadhaa wanaingia mtaani kwa usaidizi wa muongozo kutoka Base ya jeshi lililokuwa likishughulika na janga hilo.
White Spikes si tu kwamba walikuwa ni viumbe wa ajabu ila pia walikua wanajua kupigana vita. Tofauti na viumbe wengine, hawa white Spikes walikuwa na uwezo wa kukushambulia hata kwa umbali wa zaidi ya mita miamoja. Kwa ufupi tu muziki wa hawa viumbe ulikuwa ni next level mazee.
Mission ya awali kabisa ilikuwa ni kuvielekeza vikosi vyote kuelekea ilipokuwa Lab ya kijeshi iliyokuwa inafanya tafiti mbali mbali ili kuweza kupambana na viumbe hao na kilichotakiwa kuchukuliwa kutoka Lab hiyo kupelekwa katika Lab nyingine salama ilikuwa ni ile sampuli ya utafiti ambayo ilikuwa ikiendelea kufanyiwa majaribio.
Malkia wa White Spikes akiongoza jeshi kubwa la Spikes anatoa ishara ya kufatiliwa wakiana Dan baada ya wao kufanikisha kupata sampuli hile japokuwa walikuta Lab imeharibiwa na watu wengi wakiwa wamepoteza maisha. Nje ya Lab na katika korido za ngazi katika jengo hilo wamejaa White Spikes wakiendelea kudumisha Doria 😀.
Nini ilikuwa hatima ya kina Dan..!?, Je Dan aliweza kurudi kuungana na familia yake tena..!?, Iliwezekana kuwamaliza White Spikes wote..!?, Haya yote maswali yatamalizwa kwa kuijipa muda na kuitazama Filamu hii bomba kabisa.
Niandikie Filamu unayopenda tuje na uchambuzi wake ila zingatia Filamu hiyo iwe na kuanzia rate ya 5/10. Kula chuma hicho....!!!
#Tufollow
#BestMovie
#ShareLike