Tamaduni ya mume kuishi ukweni

ALEX_ANDER

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2014
Posts
570
Reaction score
828
Umuofia Kwenu?

Katika kuishi kwangu Visiwani Comoros, nilipata kuona tamaduni moja ya maisha ya ndoa. Mwanaume unaenda kuishi kwa mwanamke yaani nyumbani kwenye familia ya mke.

Yaani ipo hivi, Baba anatakiwa kuhakikisha kwenye kaya yake kunakuwa na miliki ya makazi (mara nyingi ni chumba na sehemu ya kujitosheleza) au floor nzima kwa ajili ya binti yake au mabinti zake.

Ambapo anapofika muda wa kuolewa, mume huja kuishi na mke hapo. Kama baba amefariki, basi kaka, mjomba ndio watahusika kwa hilo.

Mambo ya kila siku ya kifamilia ya binti huwa yako kwa binti na mume wake.

Na inapotokea wameachana, mume huondoka na kurudi kwao.

Wenyewe wanadai ina faida juu ya kuzuia unyanyasaji wa wanawake.

Je wewe hii unaionaje?
 
Mfumo wa utoaji mahari kwao ukoje mkuu.

Kingsmann

Kiutamaduni mahari, ndoa na harusi uko hivi
Mahari huwa ni dhahabu( wana kipimo maalum ambacho nimesahau), mavazi na pesa mwanaume ndiye mtoaji

Ndoa mara nyingi zinafungwa msikitini, wana mavazi yao special ya kitamaduni kama majoho kwa wanawake na kanzu, kofia na vikoti kwa wanaume.

Harusi- ziko za aina mbili

1.Harusi ya kawaida (marriage normalle) --
Hii hufanyika siku ya kufunga ndoa au siku chache kwenye wiki ya ndoa.

2.Harusi kubwa (Grande marriage) au Ardaa
Hii ni sherehe ya harusi ambayo ni ndoto ya wengi kwani humpa mtu heshima ndani ya jamii yao, na hata kuna namna ya uvaaji w watu waliowahi kufanya harusi hii.

Hii ni sherehe ambayo inaweza kufanyika week nzima kwa mpangilio wa matukio mbali mbali.
Na huwa inaalika watu wengine kutoka kila kona ya kisiwa, mtu mmoja niliwahi muuliza gharama alinambia alitumia around 50,000€ kwenye tukio zima.
 
du, yaani eur 50000,
 
Iyo sehemu kwamba baba akifariki kaka anarithi nyumba, inamana huyo kaka ha o i
 
Hii kwa jamii yetu itakuwa ni ngumu kidogo,wanaume wa huku kwetu tunahitaji ka uhuru flani hivi...
 
Iyo sehemu kwamba baba akifariki kaka anarithi nyumba, inamana huyo kaka ha o i

Sio kama Kaka anarithi bali Kaka anasimamia kile alichotakiwa kukifanya Baba kwa ajili ya binti
 
Sasa mkizaa watoto na wakakua nao wakataka kuolewa na wewe unaishi kwa wakwe hapo inakaaje? Wakwe wanahama kupisha wajukuu kuolewa au niaje? Au unaishi pale kwa muda then utahama kwenda kutafuta mji wako?

Mbona haijakaa sawa kihesabu.
 
Sasa mkizaa watoto na wakakua nao wakataka kuolewa na wewe unaishi kwa wakwe hapo inakaaje? Wakwe wanahama kupisha wajukuu kuolewa au niaje? Au unaishi pale kwa muda then utahama kwenda kutafuta mji wako?

Mbona haijakaa sawa kihesabu.

Wakati mnaendelea kuishi, nyumba zao nyingi huwa zina matoleo ya ghorofa yaani kama hazijamaliziwa hivyo huruhusu mtu kuendeleza kujenga ila nilipata kuona wengine ambao umri umeenda na waliojaliw kipato kama wanandoa wanajenga mji mwingine kwenye maeneo ya familia, wakilenga kuwawekea binti binti zao au binti wa ndugu zao.
 
Uzuri wa tamaduni haina athari kwa yule aliyezaliwa akaikuta kwasabu unakuta misingi mingi imewekwa kwa mwelekeo huo...

Ni sawa na useme Tz wanaume walipiwe mahari kama wahindi.. Ila wao wanaona sawa tu..

Japo kuishi ukweli sio poa kabisa,,, kwa hapa kwetu utasimangwa sana na mke atakudharau pia vile hatujalelewa kwa misingi hio.
 

For sure they are very comfortable afu wanakupa sababu ambazo ukiwasikiliza na life style yao "Umwinyi" utaona sawa [emoji23][emoji23]
 
Wahindi ndo mila zao hizi yaan tena mwanaume anatolewa mahari na mwanamke na anaenda kukaa ukweni .Hili jambo ni zuri sana wanakaa kwa mapenzi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…