Tamaa ni mbaya. Angalia kilichomkuta huyu

Mangungu

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
2,392
3,017
Habari za asubuhi wananchi wenzangu.

Mimi ni kijana Mtanzania, mwajiriwa serikalini, mwenye miaka 35,nina watoto wawili na huyu mke wangu, ambaye nilifunga nae ndoa mwaka 2016, japo ni ndoa ya bomani na wala sio ya kanisani! Mimi na mke wangu tulipendana sana miaka ya nyuma, hakuwa msiri kwenye mambo yake,wala sikuwa msiri kwenye mambo yangu, simu yangu na email yangu vilikua vyake, pia simu yake na email yake vilikua vyangu.

Mwaka 2017 nilienda nje ya nchi kikazi nilikaa huko yapata miezi 8 hivi, wakati huo mtoto wangu wa pili alikua na miaka 3,nilikua napenda sana kupiga video call, naongea na wanangu, lakini kuna siku wife akawa hapokei video call, tena wakati huo ni usiku saa mbili au saa tatu hivi. Na akaanza tabia, hadi apige yeye ndiyo nitaongea na wanangu.

Ukija uliza anasema alipitiwa na usingizi,kumbe aliondoka na kwenda kwa bwana wake,watoto anawaacha wakiwa wamelala na Dada wa kazi. Kuna siku alituma sms ya WhatsApp, kua ile email hatumii tena, ana email mpya. Nikaomba password akaninyima. Nikasema poa!

Basi mwezi wa pili mwaka 2018 nikarudi Tanzania, sikuwa na hili wala lile,siku moja akasema amepata kazi Simiyu,nikauliza ofisi gani, hakutaja jina,bila ya kua na aibu wala soni machoni akaniaga anaenda kufanya kazi,nikasema haina shida,maana niliona acha na yeye akapambane na maisha,ili mikono miwili iweze kujenga!

Kweli baada ya mwezi,akaanza safari, nikasema nimsindikize akasema hapana wewe kaa na watoto kwanza, hapo machale yalikua yashaanza kucheza, maana kuna siku akipigiwa simu tuko pamoja, anagoma kupokea.

Basi akaenda zake Simiyu, baada ya week moja nami nikaenda Simiyu, chakushangaza,nilikuta kuna mambo mengi sana nyumbani kwake, ana vitu vya dhamani kubwa sana, nikauliza kulikoni, akasema kapewa mkopo ofisini kwao, ofisi gani hataki kusema. Mkopo gani jamani hata miezi miwili ofisini hajamaliza? Ofisi gani hii inatoa mikopo mikubwa hivi ndani ya mwezi mmoja tu? Nikasema hapana kuna jambo hapa.

Siku moja bado nikiwa hapo kwake,nikaona simu mpya ndogo,na alikua na line mpya,ambayo mimi hata siijui, nikaichukua ile simu nakuanza kusoma sms za mle ndani, wadau kidogo nipate kichaa cha maisha. Niliumia sana, kumbe ana bwana mwingne wameanza tangu Mimi nikiwa safari nje ya nchi. Sikuwahi kulia, ila that day nilitoa machozi mwanaume mimi, niliwaza wanangu, ndugu zangu, na watu walio karibu yangu, nikasema hivi kama ningekua na gun hapa, si mambo yangekua mengine kabisa, maana gun niliacha home, wanapanga hadi mimi anichokoze, nimpige apate nafasi yakuvunja ndoa ili akaolewe na huyo bwana wake. Aliporudi toka kazini kwake, kusikojulikana aliniuliza unaondoka lini? Nikasema hata sasa hivi, basi nikaichukua ile simu, nikaondoka nayo bila ya yeye kujua, huwezi amini, hata kunisindikiza stand hakwenda.

Nikiwa njiani, ikaingia sms kutoka kwa jamaa, anauliza, vipi huyo pimbi, anaondoka lini, maana nina safari yakuja mwanza, nitapita hadi kwako, wife naye akanipigia simu, hata kabla sijafika stand, akauliza kuna simu yangu hapa, umeondoka nayo? Nikajibu ndiyo! Alikata simu, akaja hadi stand, akaomba nimpe simu yake, niligoma, nikamwambia tena naweza mpa kipondo kizito ili tuachane vizuri akaolewe na huyo jamaa yake!

Nikasema hapa mimi na yeye tushaingia kwenye ugomvi mzito sana, nika copy zile text zote from sim card to phone! Maana nilijua akienda renew line nitapoteza ushaidi wangu! Na kweli alifanya hivyo!

Nikarudi zangu hadi nyumbani kwangu, nikamwita kaka yangu,nikamweleza mambo yote, alichonishauri ni kwamba, tuliza akili achana nae, kweli nikatuliza akili, but nilipata stress sana, nikawa nalewa sana, narudi nyumbani saa saba usiku, hadi nikaomba likizo kazini, boss wangu ni mwelewa sana, baada yakumweleza mkasa mzima, alinipa 56days zakutuliza akili, maana ilikua nife au nipate hata ajali kabisa. Watoto kila siku wanauliza mama yuko wapi? Atarudi lini? Huyu shwain, kwa mda wote huo hajawahi piga simu kuuliza kuhusu watoto wake. Visa vikaendelea, siku moja nilipiga simu kwa mama yake, nikamweleza, mama yake huwezi amini alifunguka mambo mengi sana kuhusu mwanae, aliniambia neno moja tu, mwanangu tuliza akili, hakuna jambo lisilo na mwisho, najua mke wako atakuja kwako analia nakuomba samahani.

Basi nilikaa na wanangu, na yule mdada wa kazi, dada wa kazi anawapenda sana wanangu, sijawahi ona dada kama huyu,tangu 2018 mimi na huyu mwanamke tulikata mawasiliano kabisa, nikawa naongea na mama yake tu. Bidada hakujua kua yule jamaa ana mke wake na watoto, katika tumbua tumbua za Magu, jamaa akapitiwa bwana, jamaa akarudisha majeshi kwa mke wake, bidada akakosa misaada kedekede zakutoka kwa jamaa, bidada akarudisha majeshi home kwao, baba na mama wakamtimua, kama paka mwizi, akaenda domu kwa mdogo wake, shemeji yake mme wa mdogo wake akamtimua pia, kua anaweza mfundisha ujinga mke wake. Basi last week Mama mkwe alinipigia simu, akaniambia Baba nilikuambia tuliza akili, sasa umeona yaliyomkuta mke wako? Akanipa full story, mama akashauri mwanangu, hayo mambo ni yako wewe na mkeo, mkiyamaliza sawa, mkishindwana sawa!

Kaka pia kanipandia hewani,kanipa mkanda wote,akasema dogo komaa, Juzi bidada kapiga simu,anauliza wanangu wapo? (Mungu anisamehe nilisema walishakufa toka 2018) Anaomba maongezi na mimi, nikajibu kwani Jonh yuko wapi?? Hadi sasa hivi anapiga simu Mara ishirini kwa siku, sms ndo nyingi tu, sasa nimempiga block kote kote,Sms,Call,WhatsApp na IG!

Wanawake kwa nini mnakua na tamaa za maisha ya mda mfupi? Unaweza jenga nyumba baada ya 10 years, unaweza nunua gari baada ya 5 years baada yakuanza kazi! Acheni tamaa,mnavunja ndoa zenu wenyewe!
 
Kwanza huyo kisheria bado mkeo maana hujavunja ndoa mahakamani. Kama kweli humtaki nenda mahakamani uvunje ndoa vinginevyo ukifa hata miaka 20 ijayo ataibuka na kudai yeye ni mke halali na atarithi mali yote na kwa hasira anaweza hata kuwadulumu wanao/ wanae.

Inaonyesha wewe ni dhaifu na huwezi kumuacha ndio maana unaingiza siasa katika ndoa.
Suka au nyoa
.
 
Mkuu, pole sana na mkasa huo mzito. Kwanza, si wanawake wote wako hivyo huyo wako kidogo amekengeuka. Pili, msamehe, msamaha utakufanya uwe huru na amani ya moyo.Tatu, ni uamuzi wako sasa kumrudia au kuachana nae moja kwa moja kupitia talaka ya mahakamani.Mwisho, mwanamke pekèe unayepaswa kumuamini ni mama yako mzazi.
 
Kwanza huyo kisheria bado mkeo maana hujavunja ndoa mahakamani. Kama kweli humtaki nenda mahakamani uvunje ndoa vinginevyo ukifa hata miaka 20 ijayo ataibuka na kudai yeye ni mke halali na atarithi mali yote na kwa hasira anaweza hata kuwadulumu wanao/ wanae.
Inaonyesha wewe ni dhaifu na huwezi kumuacha ndio maana unaingiza siasa katika ndoa.
Suka au nyoa
.
Tatizo hunijui!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom