Ken ni daktari katika moja ya hosipitali za serikali hapa mjini, ni mtoto wa mwisho kuzaliwa katika familia ya watoto wanne na akiwa mtoto pekee wa kiume.
Baba yake alikua ofisa wa ubalozi Diplomat na alifanya kazi katika nchi nyingi duniani. Dada zake Ken walichangia sana katika malezi ya mdogo wao wa mwisho hasa baada ya wazazi kustaahafu.
Madada wote wameolewa na wanamaisha ya kawaida ila dada mkubwa ambae kutoka na wadhifa wa mume wake na biashara zake mwenyewe pesa imemtembelea vibaya sana. Ken alikutana na binti mmoja, mrembo wa haja akiwa anasoma kidato cha sita katika shule ya kutwa.
Ken alichanganyikiwa kwa urembo wa binti alimueleza binti nia yake ni kutaka kumuoa na angependa awafahamu wazazi wake ili adhihirishe nia yake.Binti alitoka katika familia ya kawaida sana, basi aliwafahamisha wazazi wake, na Ken alikwenda kujitambulisha na kutoka hapo, mahitaji mengi ya binti Ken aliyahudumia.
Baada ya binti kufanya mtihani wake wa mwisho, posa ilipelekwa, na mipango ya ndoa ilianza. Baada ya harusi, dada mkubwa aligharimia honeymoon yao London kwa wiki mbili na baada ya hapo maisha yalianza kama mke na mume.
Madada wa Ken wakiwa na ufahamu wa mambo mengi well exposed, walianza kumfundisha wifi yao mambo mengi ambayo hakuyafahamu, e.g.
Jinsi ya kuandaa meza wapi inakaa glass ya maji, red wine, white wine, kisu cha nyama steak, kisu cha samaki, starter plate, e.c.t. Hawakutaka kaka yao aaibike akipata wageni.
Dada mkubwa kutokana na biashara zake alisafiri nchi nyingi mara kwa mara, na kila akirudi alimletea perfume Binti mambo ya Gucci, Estee Lauder, Lancôme, Channel ect.
Kwakweli alimchukulia kama mdogo wake, basi akawa anamfundisha kuwa mwanamke unatakiwa uwe na hata hand bag moja nzuri ya kutokea mbele za watu, dada akamletea na hand bag ya Louis Vuitton hand bag pamoja na wallet yake.
Binti alipoonjeshwa mambo mazuri si utamu ukamkolea, siku ya siku mume wa dada mkubwa alimwambia wewe ni mzuri sana, unatakiwa kupata mwanaume kama mimi, huyu Ken hana pesa ya kukuhudumia wewe.
Alipewa number ya simu, Binti alikua na akili zake, alitafuta handset na line nyingine ndiyo alikua anawasiliana na buzi lake, mapenzi yakakolea.
Walikua wanakutana hotelini,basi mmoja wa wahudumu wa hoteli kwa kujipendekeza, alimtafuta dada mkubwa ambae ndiye mke akamueleza ishu inavyoendelea, dada alimpa number yake ya simu.
Akamwambia ukimuona mume wangu anakuja hotelini kwenu nipigie simu, wakati wote huo hakujua kua mwizi wake ni wifi yake.Alipomfumania wifi yake.
Basi alimueleza Ken, Ken alichanganyikiwa alimwambia binti, sihitaji kukuona sitarudi hapo nyumbani mpaka baada ya siku tatu na nikirudi nisikukute.