Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Kundi moja lililojitenga kutoka kwa wapiganaji wa Taliban limesema ndilo lililotekeleza shambulio la kujitoa mhanga mjini Lahore, Pakistan lililoua watu zaidi ya 70.
Kundi hilo la Jamaat-ul-Ahrar lilisema liliwalenga Wakristo waliokuwa wakisherehekea Pasaka, ingawa polisi wamesema bado wanachunguza madai hayo.
Kulikuwa na hali ya kutamausha wazazi wakiwatafuta watoto wao kwenye vifusi.
Rais wa Pakistan ameshutumu shambulio hilo na serikali ya jimbo imetangaza siku tatu za maombolezo.
Takriban watu 300 walijeruhiwa, na maafisa wanasema idadi ya waliofariki inatarajiwa kuongezeka.
Mlipuko huo ulitokea kwenye bustani ya Gulshan-e-Iqbal mjini Lahore karibu na eneo la kuchezea watoto Jumapili jioni.
Lahore ni mji tajiri na ni mojawapo wa miji yenye mtazamo huru zaidi nchini Pakistan.
Ndiyo ngome ya kisiasa ya waziri mkuu wa sasa Nawaz Sharif, na haujakuwa ukishuhudia mashambulio mengi ya kigaidi miaka ya karibuni.
Msemaji wa kundi la Jamaat-ul-Ahrar, Ehsanullah Ehsan, alisema kundi hilo lilitaka kutuma ujumbe kwa Bw Sharif kwamba wameingia Lahore na akasema kundi hilo litatekeleza mashambulio zaidi.
Jamaat-ul-Ahrar walijitenga kutoka kwa Tehrik-e Taliban Pakistan. Limetekeleza mashambulio mengine kadha dhidi ya raia na vikosi vya usalama miezi ya hivi majuzi.
Bw Sharif ameeleza masikitiko yake na huzuni kutokana na watu wengi wasio na hatia waliopoteza maisha yao.
Ameahirisha ziara aliyokuwa amepanga kuifanya nchini Uingereza.
Source: BBC