TAKWIMU: Nini kimepelekea Mitandao ya tiGO na Zantel kupoteza wateja na Vodacom kupanda?

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
Wakuu,

Namba hazidanganyi. Siku za nyuma tulizoea kuona mtandao wa Mobitel/Buzz/tiGO ukiwa mbele kwa idadi ya subscribers lakini siku za hivi karibuni hali imekuwa tofauti kabisa.

1ed4a781c0ae9f335a45955a0ec9c4a2.jpg

25301042f98b6204d234e1b01afbd141.jpg


Kwa mujibu wa TCRA, hali inaonekana kuwa si nzuri kwa wateja wa mtandao huo imeshuka tofauti na Wenzao Vodacom ambao wanaonekana kufanya vyema upande huu.

Je, ni mdororo wa kiuchumi?

Je, ni mabadiliko ya kiteknolojia na usikivu wa mawasiliano?

Je, ni huduma mbovu zinazopelekea wateja kuhamia mitandao mingine wakitafuta kilicho bora?

Je, siku za nyuma walikuwa wakidanganya juu ya idadi ya subscribers wao na sasa wanalazimika kutoa figure sahihi?

Au ni gharama kupanda na kupelekea wateja kuukimbia mtandao?
 
Generally wateja wote wamepungua in terms of voice ila data za ujumla kwa wateja waliosajiliwa kwenye mitandao.

Vodacom hawana cha kujivunia ni market leader ambae anashuka kila siku compared to tigo ambao kila siku wanapanda now ni wa pili na kwa mwaka wamefikia kitu kama 29% of market share pulling down the share for Vodacom na Airtel ambao ni wazi wanaelekea kuzimu
 
Mtandao wa tiGo umenunua Zantel so kwenye idadi bado tigo anaongoza kuongoza zaidi ya Vodacom kwa wateja wengi.

Ila kiuhalisia, Vodacom ndo mtandao reliable kuliko hao wengine. Sijaona wa kushindana nao kwenye reliability.
 
Voda siyo reliable wanabadiri vifurushi bila taarifa

Pili mtandao wao wanaminya spidi, kiasi kwamba ndani ya masaa 24 ukisubscribe vifurushi hivyo, kuna point mtandao unakuwa slow mno kiasi kwamba huwezi kuzitumia bando zako walizokwambia wanakupa.

Tatu voda vifurushi vyao ni ghali mno.

Mimi nina laini mbili, huwa ninatumia bando za kampuni nyingine kabla sijafikiria kutunia voda!
 
Voda siyo reliable wanabadiri vifurushi bila taarifa

Pili mtandao wao wanaminya spidi, kiasi kwamba ndani ya masaa 24 ukisubscribe vifurushi hivyo, kuna point mtandao unakuwa slow mno kiasi kwamba huwezi kuzitumia bando zako walizokwambia wanakupa.

Tatu voda vifurushi vyao ni ghali mno.

Mimi nina laini mbili, huwa ninatumia bando za kampuni nyingine kabla sijafikiria kutunia voda!
Kwenye data vodacom hawana mpinzani wapo vizuri. Kuhusu gharama ni kweli bundles zao ni ghali kulinganisha na wengine. Pia nikweli wanabadili huduma zao bila kutoa taarifa. Hapa wanakera sana.

Miaka yote Vodacom ndiyo leading network provider kwakuwa na wateja wengi. Nimeangalia nimeona Vodacom bado wanaendelea kuongeza wateja ilhali makampuni ya Tigo na Zantel wanashuka.

Halotel wapo very cheap. Naniaona wanapanda taratibu. Data speed yao sio mbaya.....huwa natumia once in a while nikiona Vodacom wanaleta zakuleta.

Smart sijawahi tumia......nitajaribu soon
 
Lakini huoni kama total subscribers wamepungua December kulinganisha na October?
 
Tatizo ni gharama za bando la tigo liko juu. 650 unapata dakika 6 kupiga mitandao yote wakati mtandao kama Halotel kwa 649 unapata dakika 14 za kupiga mitandao yote. Ni lazima watu wahame wakatafute unafuu wa huduma.
 
Sasa ivi ukiongelea hii mitandao asilimia kikubwa watu wapo katika data., Vodacom ni best kwa sababu hadi sasa ni mtandao pekee ambao kwa mtazamo wangu upo consistence kwenye speed yake tofauti na kina halotel ambao walikuja kwa fujo lakin customers walipoongezeka mtandao ukazidiwa wakaanza kupwaya customers wakakimbia.

Tigo kwa uzoefu wangu naturally hawako vizuri kwenye data labda niseme hawako vizuri maeneo mingi nchini ni baadhi tu ya maeneo ya mijini sasa inakuwa shida ku access., labda kwenye tigopesa wanafanya vizur.

TTCL wao wamejisahau kama biashara wanayoifanya ni kwa watanzania maskini kila kitu kwao bei ipo juu sana nadhan lengo lao zaidi wana invest kwenye majengo ya serikali na watu wenye vipato vya juu sio individual customers. Juzi wamekuja na 4G lakini speed ni afadhali ya 3G ya vodacom.

Mtandao wa mwisho kabisa Tz ambao unasuasua tokea uanzishwe ni Zantel, tokea kwenye voice data na kila kitu ni usumbufu wa hali ya juu kabisa hawako vizuri nawachukia hadi wale customer care wao viburi mtindo mmoja.
 
Kinachowabeba voda ni m-PESA na si kingine. Imejikita kuwapa mawakala wao commission kubwa.

Kama ukifuatilia ukienda kwa wakala ukiulizia kutoa TIGO PESA kiasi kikubwa utaambiwa hakuna but ukisema M-PESA unambiwa toa so market intelligence needed
 
Vodacom dhambi ya kutoa Siri za wateja wao (kesi ya Lema ) itawatafuma na watapotezwa kabisa
 
Back
Top Bottom