1. Baada ya mtuhumiwa kukamatwa pale st.Gapar, je alisafirishwa hadi Dsm?
2.Mtuhumiwa alipotua pale airport chini ya escort ya polisi wakiwa na mabegi yenye fedha za ushahidi, je aliwekwa mahabusu kituo cha jirani, kwa mfano pale stakishari na kidhibiti kikafungiwa stoo?
3.Kama siri za mpango huo zilivujishwa kwa mwenye mzigo, je aliamua kutuma kikosi chenye silaha kufuata mabegi yenye fedha stoo ili kupoteza ushahidi mahakamani?
4.Tukio la uvamizi wa kimafia kituo cha polisi sitakishari, lilikuwa na lengo la kupora silaha tu, au pamoja na kupoteza ushahidi stoo?
5.Unganisha nukta....mtoto hatumwi dukani bila hela, na mwenye hela anajua hela yake ilipo!
Usilolijua ni usiku wa giza, si kila tuhuma ni kosa la jinai. Kwanza unatuchanganyia habari, nadahani huna uelewa mpana wa haya mambo. Tukio la Stakishari halina uhusianoi wowote na tukio la kukamatwa kwa mabegi ya fedha Dododma. Tukio la Sitakishari ni tukio linalotia simanzi, askari wetu wanne pamoja na raia watatu kuuawa kinyama tuachie vyombo vya ulinzi na usalama vilisgughulikie. Polisi wamekwisha sema mtu yeyote mwenye taarifa zinazoweza kusaidia kukamatwa kwa wale majambazi apeleke polisi na zawadi kubwa imeahidiwa kwa hilo, mwenye taarifa na azipeleke polisi sisi wengine tusiyokuwa na taarifa basi na tukae kimya tuache vyombo vinavyohusika kulifanyia kazi.
kuhusu pesa zilizokamatwa Dodoma, kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma kisha tolea taarifa, anasema kama hukusikia uchunguzi uliofanywa na polisi umegundua kwamba zile ni pesa halali na wala hazuina uhusiano wowote na maswala ya rushwa, hivyo mtuhumiwa kaachiwa na kurudishiwa pesa zake. Waswahili watasema mengi, lakini taarifa ya polisi ambao kimsingi hiyo ndiyo shughuli yao wamekwisha kusema mtuhumiwa ameachia na kurudishiwa pesa zake, asasa wewe kama una taarifa yeyote kinyume cha hapo basi wapelekee pamoja na ushahidi ulionao, kinyume cha hapo ya Ngoswe muachie Ngoswe.