Takukuru yawasaka Mungai, Mwakalebela

Takukuru yawasaka Mungai, Mwakalebela

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803

NA GODFREY MUSHI

3rd August 2012

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inawasaka makada wawili wa CCM, Waziri wa zamani, Joseph Mungai na Katibu Mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela, kutokana na kukabiliwa na tuhuma za rushwa katika chaguzi za Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mungai anakabiliwa na tuhuma za utoaji rushwa kinyume cha sheria ya Takukuru ya mwaka 2007 na sheria ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010.

Kaimu Kamanda wa Takukuru mkoa wa Iringa, Stephen Mafipa, alisema kuwa Mungai na Mwakalebela wanatafutwaili wafikishwe upya mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili, baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa kutupilia mbali rufani zao.

Mungai na wenzake wawili walikuwa wakiiomba Mahakama Muu kutolea uamuzi hoja mbili ambazo Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoa wa Iringa ilishindwa kutolea maamuzi katika kesi ya msingi.

Hoja ya kwanza kwa mujibu wa Mungai ni kwamba makosa yote 15 aliyoshitakiwa yeye na wenzake siyo ya jinai kutokana na kukosa maneno muhimu kisheria kama inavyotakiwa sheria namba 11 ya Takukuru ya 2007.

Aidha, taarifa hiyo inaitaja pia hoja ya pili ambayo imetupiliwa mbali na Mahakma Kuu ni kifungu cha 21 (1) (a) na kifungu cha 24 (8) cha sheria ya gharama za uchaguzi namba 6 ya mwaka 2010 ambacho Mungai na wenzake wanadai hakitengenezi kosa la jinai.

Awali, Mungai na makada wengine wawili wa CCM, akiwemo Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Mufindi, Fidel Cholela (41) na Moses Masasi walikuwa wakikabiliwa na mashtaka 15 ya kutoa rushwa na sheria ya gharama za uchaguzi ya mwaka 2010.

Inadaiwa kuwa Julai 08, mwaka huu, katika Kata ya Ihalimba, Wilaya ya Mufindi, Mungai na watuhumiwa wenzake walitoa hongo ya Sh.10,000 kwa Mwenyekiti wa CCM tawi la Vikula kama kishawishi cha kumpigia kura wakati wa zoezi la upigaji wa kura za maoni.

Mwakalebela anakabiliwa na tuhuma za rushwa katika chaguzi za CCM zilizofanyika mwaka 2010 wakati wa mchakato wa kura za maoni Jimbo la Iringa Mjini.

Mwakalebela anadaiwa kutenda kosa hilo Juni 2010 katika Kijiji cha Mkoga, Manispaa ya Iringa ambapo anadaiwa kutoa hongo ya Sh.100,000 kwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Hamisi Luhanga ili azigawe kwa wapiga kura 30 wa CCM ili wampigie kura.


CHANZO: NIPASHE
 
Waacheni Jamani Kuna Wezi Zaidi yao na Wanaendelea na Wizi wao Ndani ya BUNGE yaani Chombo Cha kutunga

Sheria za Nchi...
 
neno 'kusaka' aghalabu linafaa zaidi mfano pale unapomtafuta panya aliyejificha kwenye stoo iliyojaa mavitu kibao. Lakini sio kama panya anaonekana, tena katulia sehemu ya wazi, na wala hakimbii.
 
Wanawake wawili watoto wazuuuriii nimemaliza ss hv
 
Ukila rushwa ni sawa na kula nyama ya mtu...acha wakanyee debe ili wajifunze...big up sana TAKUKURU kwa kazi yenu nzuri...ila msiishie hapo kazeni uzi zaidi...
 
wanasakwa kwani wapo mafichoni?kwanza hata wakiitwa wanakuja achilia mbali kuwafuata na kuwashika bila kutafuta.Mbona kauli kama vile ni zoezi humu.Nakumbuka issue za polisi wanavyouwa wanaominika kuwa wahalifu tena katika ambush baada ya kutonywa na wanaoaminika kuwa raia wema(majambazi waliokosa mgao).Basi huwa utasikia polisi wameua majambazi sugu katika mapambao ya kubarushiana risasi katika mapambano ya masaa zaidi ya 8. Masaa 8 katika mashambuizi hata ubongo hupungua concentration na mtu kuingia katika fatigue na hakuna uwezekano wa hata polisi kutoka salama wakati wengine wamekufa.othewrise kama polisi walikuwa wamelindwa na bullet proof ,sijui na gesi mask.Basi katik ahiyo vita majamabazi wasingetumia hata saa1 bila kuuawawa.
 
wanasakwa kwani wapo
mafichoni?kwanza hata wakiitwa wanakuja achilia mbali kuwafuata na
kuwashika bila kutafuta.Mbona kauli kama vile ni zoezi humu.Nakumbuka
issue za polisi wanavyouwa wanaominika kuwa wahalifu tena katika ambush
baada ya kutonywa na wanaoaminika kuwa raia wema(majambazi waliokosa
mgao).Basi huwa utasikia polisi wameua majambazi sugu katika mapambao ya
kubarushiana risasi katika mapambano ya masaa zaidi ya 8. Masaa 8
katika mashambuizi hata ubongo hupungua concentration na mtu kuingia
katika fatigue na hakuna uwezekano wa hata polisi kutoka salama wakati
wengine wamekufa.othewrise kama polisi walikuwa wamelindwa na bullet
proof ,sijui na gesi mask.Basi katik ahiyo vita majamabazi wasingetumia
hata saa1 bila kuuawawa.

hiyo taarifa ilitolewa baada ya pingamizi zao kutupwa mahakama kuu.
 
Takukuru ni mzigo kwa walipa kodi wa Tanzania. Hawana la maana wanalofanya
 
Back
Top Bottom