TAKUKURU: Tulimkuta Mhadhiri wa NIT guest akiwa mtupu akiomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wake

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Messages
2,210
Points
2,000

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined Apr 1, 2017
2,210 2,000
Takukuru leo Jumatano Oktoba 9, 2019 imeieleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jinsi ilivyomkuta katika nyumba ya kulala wageni mhadhiri msaidizi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Samson Mahimbo (68) akiwa mtupu.

Mahimbo anakabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya ngono kwa mwanafunzi wa chuo hicho, Victoria Faustine.

Hayo yameelezwa leo Jumatano Oktoba 9, 2019 na wakili wa taasisi hiyo ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini Tanzania, Faraja Salamba wakati akimsomea maelezo ya awali mshtakiwa huyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi.

Salamba amedai wakati wa tukio hilo mhadhiri huyo alikuwa mwajiriwa wa NIT akifundisha wanafunzi wa muhula wa kwanza wa masomo wa mwaka 2015/2016 somo la usimamizi wa barabara na usafirishaji.

Amedai Januari 5 na 11, 2017 mshtakiwa alitumia madaraka yake vibaya kwa kuomba rushwa ya ngono na alimpigia simu Victoria na kumsisitiza wakutane katika baa ya Shani.

Amedai walipokutana mshtakiwa huyo alikuwa na mtihani wa Victoria wa marudio wa somo alilokuwa akimfundisha na majibu, alimpa aufanye na alipomaliza akasahihisha na kumpa alama 67.

Imedaiwa kuwa baada ya Victoria kumaliza kufanya mtihani huo na kusahihishiwa walihamia baa nyingine ya Camp David na kunywa pombe na mshtakiwa kuchukua chumba.

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa walipoingia chumbani mshtakiwa alivua suruali na kupaki na nguo ya ndani na kumkumbatia mwanafunzi huyo.

Salamba amesema wakati mhadhiri huyo akimvua nguo mwanafunzi huyo mlango uligongwa na Victoria alikwenda kufungua na waliingia maofisa wa Takukuru

“Waliingia maofisa wa Takukuru, mjumbe na mhudumu wa Baa na kukuta nguo za mshtakiwa juu ya meza,” amesema Salamba.

Wakili huyo wa Takukuru amedai Januari 12, 2017 mshtakiwa huyo aliandika maelezo Takukuru na Agosti 14, 2019 alifikishwa mahakamani.

Katika kesi hiyo upande wa mashtaka unatarajia kuita mashahidi sita na kuwasilisha vielelezo saba.

Baada ya kusomwa kwa maelezo hayo, mshtakiwa alikubali maelezo yake na kukana shtaka linalomkabili.

Kesi itaanza kusikilizwa Novemba 4, 2019 kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.
Katika kesi hiyo mhadhiri huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 12, 2017 katika nyumba ya kulala wageni ya Camp David iliyopo Mlalakuwa Mwenge.

Ilidaiwa akiwa mwajiriwa wa NIT kozi ya usimamizi wa barabara na usafirishaji namba LTU 07101 kwa kutumia mamlaka yake alimlazimisha mwanafunzi huyo kutoa rushwa ya ngono.

Anadaiwa kuomba rushwa hiyo ili aweze kumfanya mwanafunzi huyo kufaulu mtihani wake wa marudio katika kozi ya usimamizi wa barabara na usafirishaji uliokuwa unafanyika Januari 5, 2017.

Mshtakiwa huyo yupo nje kwa dhamana na alikana mashtaka yanayomkabili.

SOMA PIA:


 

CABANA

Senior Member
Joined
Feb 6, 2013
Messages
195
Points
250

CABANA

Senior Member
Joined Feb 6, 2013
195 250
Duh... Ni hatari.....mabinti hawataki kusoma wanapenda mtelezo... Huyo mzee kesha wapitia wangapi mpaka arobaini ikamfika...

Hapo Camp David inaonekana ni mahali pa uasherati....sheria zinasemaje kama vipi pafungiwe na penyewe iwe kama Zenji.. Bila cheti cha ndoa hamlali chumba kimoja ke na me.
 

KWEZISHO

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2016
Messages
7,543
Points
2,000

KWEZISHO

JF-Expert Member
Joined Jan 29, 2016
7,543 2,000
Jamaa huyu hapa. Sasa akiwa uchi wa mnyama anakuwaje hapo... View attachment 1227576
Yawezekana ni kweli ametenda au yawezekana hajatenda. Huyu ni mtuhumiwa na sio mhukumiwa. Hii dunia kuna vitu vingine vinahitaji kupewa nafasi kabla hukumu. Tusiwe wepesi kuhukumu. Tusubiri utetezi wake na atakavyosikilizwa na mahakama.
 

Kambaku

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2011
Messages
2,866
Points
2,000

Kambaku

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2011
2,866 2,000
Acheni kudhalilisha watu aisee, huyo mtu anafamilia, sasa ulienda guest kufanya nn kama ulikuwa hutaki, si ungefabya limtihani lako kivyako..
Inawezkana alikwenda gesti huyo dada ikiwa ni sehemu ya mtego mkuu. Unadhani alikuwa hajui huyo dada kama Takukuru watakuja kugonga? Na ni lazima ni yeye mwenyewe (dada) ndio aliripoti huko Takukuru
 

Farolito

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Messages
2,941
Points
2,000

Farolito

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2018
2,941 2,000
Wangempiga na picha kabisa akiwa Gest,
Juzi kuna mhadhiri mmoja wa Ghana kaumbuliwa na mwandishi undercover wa BBC alijifanya mwanafunzi anaomba udahili kaingia Kingi,halafu alikuwa mchungaji,Sasahivi nadhani keshafukuzwa
 

Forum statistics

Threads 1,379,308
Members 525,379
Posts 33,742,249
Top