TAKUKURU: Polisi wanaongoza kwa rushwa

TAKUKURU: Polisi wanaongoza kwa rushwa

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,156
Reaction score
64,493
Raymond Minja, Iringa



Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Iringa imetoa taarifa ya utendaji wake kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Julai mwaka jana hadi Juni mwaka huu ambapo inaonyesha polisi wanaongoza kwa kutupiwa lawama za rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa, Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Iringa, Aidan Ndomba amesema taaisisi hiyo imepokea malalamiko 142 katika kipindi cha Julai mwaka jana hadi Juni mwaka huu kati ya malalamiko hayo malalamiko 42 yamefunguliwa majalada ya uchunguzi, malalamiko 100 yamefanyiwa uchunguzi wa awali na kutolewa ushauri kwa walalamikaji.

“Idara zinazoongoza kulalamikiwa kwa rushwa Mkoa wa Iringa ni Jeshi la polisi ambapo malalamiko 20 yalipokelewa, mabaraza ya ardhi malalamiko 14,watendaji wa serikali za mitaa (kata na vijiji) pamoja na Halmashauri za Wilaya.

“Jumla ya mashauri mapya 12 yamefunguliwa mahakamani katika kipindi hicho na kufanya jumla ya mashauri 21 kuendeshwa katika mahakama,” amesema Ndomba.
 
Back
Top Bottom