Takukuru mumeshindwa kazi yenu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Takukuru mumeshindwa kazi yenu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Jethro, Aug 13, 2010.

 1. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145

  Wana JF,

  Ninapenda kusema haya machache tuu kwa wafanyakazi wa TAKUKURU, Kuwa hii kazi yao waliyoifanya kipindi cha kura za maoni naona waliishindwa 100% kwanini,

  Ntaanza na maswali machache kwao.

  Ni mgombea gani wa ccm katika kura za maoni hakutoa takrima kwa wajumbe wa ccm esp ngazi za matawi au kata??
  Kwanini nasema hilooo maana kila waandapo mikutano yao ya siri kuwa mgombea fulani anakuja kutangaza nia hujikusanya mahali na kuongea nae na pale aondokapo tuuu huwa kitu kidogo kinaachwa kutokana na idadi ya watu walio hudhuri ina kuwa kama unawalipa posho ya kikao ambacho kitaratibu za chama haipo kwani kikao kilikuwa sio halali na huwa hufanyika usiku mara kwa mara.

  Hilo TAKUKURU wanataka kuniambia hawakulijua hilo??

  Kumkamata mtu aliye toa Rushwa ya 100,000/Tsh au chini ya hapo na kutangaza kwa mbwembwe umewapeleka mahakamani esp huko Iringa me nasema kwa uwazi huo ulikuwa ni mpango madhubuti na unasimamiwa na watu fulani ili lengo lao litimizike. Haiwezakani kwa mbwembwe zenu zote TAKUKURU kutangazi vita nchi nzima kipindi cha kura za maoni na kusema watakiona cha mtemakuni bado na watu walimwaga pesa kwa kwenda mbele na nyinyi wafanyakazi wa TAKUKURU mlishiriki kupewa hongo hizo kwani zilikuwa nje nje, na mlichokuwa mkikikusanya kuhusu tuhuma za rushwa mlikuwa pia mwakipotezeshea ushahidi nyinyi wenyewe.

  Kwakweli TAKUKURU MLITIA AIBU NA SIJUI MTAENDA KUJISAFISHIA MAJI GANI WATANZANIA WAWAAMINI TENA

   
Loading...