TAKUKURU kuwasafisha akina-MKULLO?

TAKUKURU kuwasafisha akina-MKULLO?

Mkuu si unakumbuka yale ya Richmond? Takukuru ni sabuni ya kuwasafisha viongozi wanaokabiliwa na tuhuma za rushwa.
siyo richmond tu, je ya rada? hadi chenji imerudi lakini walimsafisha chenge
 
Rejea mazungumzoi ya Dr. Hosea na balozi wa Marekani yaliyovuja WIkiLeakes. "Kikwazo kikubwa cha kupambana na Rushwa KUBWA nchi hii (Tanzania) ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete"

Kama kuna Mtanzania anasubiri Mkulo, Maige, Ngeleja, Jairo, Nyoni, Ekelege etc wafikishwe mbele ya sheria! watasubiri sana hadi siku Yesu atakaporudi katika sayari hii.
 
kun thread ya jamaa mmoja anaitwa de'levis jamaa aliongea mambo mengi sana ..sasa naunganisha na haya majibu ya TAKUKURU..
 
'Ziara' zangu
ofisi za Serikali zinaelekea kubaya.Leo nilikuwa TAKUKURU ambapo mteja
wangu mmoja anahojiwa akidaiwa kula rushwa ya shilingi laki tatu ili
amwamishie mwanafunzi wake shuleni mwake.Nikawakuta maofisa wa TAKUKURU
wametingwa na shughuli zao.Uchokonozi wangu ukaiponza.Nikamtwanga swali
Afisa mmoja juu ya kuhojiwa na kupepelezwa kwa akina-MKULLO na TAKUKURU.

'Hao jamaa(Mkullo na wenzie) hawana tatizo lolote.Ni wasafi hadi
tutakapopokea maelekezo mengine toka kwa wakuu wetu.Hadi sasa hatujaanza
kuwapeleleza Waheshimiwa hao' alisema Afisa huyo. Wameanza taratibu za
kuripoti kwao kila siku? nikamuuliza. 'Waripoti ili iweje? Wakuu
hawajawapa amri hiyo.Mbona maswali yamekuwa mengi Wakili,unataka
kuwatetea nini?' alisema akiniuliza swali la kichefuchefu Afisa huyo.

Nikatamani niingie Ofisi ya Mwalimu wangu(wakati ule pale
UDSM),Dr.Edward Hossea,Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU hata nikapigane
naye.Kiukweli,nikaogopa kesi.Hadi sasa,sijui nichukue hatua gani baada
ya kukasirishwa na TAKUKURU...

wewe mwongo. kwa taarifa yako ngeleja maige na mkulo washahojiwa takukuru na uchunguzi unaendela. acha upotoshaji!
 
Back
Top Bottom