TAKUKURU kuwasafisha akina-MKULLO? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TAKUKURU kuwasafisha akina-MKULLO?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by VUTA-NKUVUTE, May 21, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  'Ziara' zangu ofisi za Serikali zinaelekea kubaya.Leo nilikuwa TAKUKURU ambapo mteja wangu mmoja anahojiwa akidaiwa kula rushwa ya shilingi laki tatu ili amwamishie mwanafunzi wake shuleni mwake.Nikawakuta maofisa wa TAKUKURU wametingwa na shughuli zao.Uchokonozi wangu ukaiponza.Nikamtwanga swali Afisa mmoja juu ya kuhojiwa na kupepelezwa kwa akina-MKULLO na TAKUKURU.

  'Hao jamaa(Mkullo na wenzie) hawana tatizo lolote.Ni wasafi hadi tutakapopokea maelekezo mengine toka kwa wakuu wetu.Hadi sasa hatujaanza kuwapeleleza Waheshimiwa hao' alisema Afisa huyo. Wameanza taratibu za kuripoti kwao kila siku? nikamuuliza. 'Waripoti ili iweje? Wakuu hawajawapa amri hiyo.Mbona maswali yamekuwa mengi Wakili,unataka kuwatetea nini?' alisema akiniuliza swali la kichefuchefu Afisa huyo.

  Nikatamani niingie Ofisi ya Mwalimu wangu(wakati ule pale UDSM),Dr.Edward Hossea,Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU hata nikapigane naye.Kiukweli,nikaogopa kesi.Hadi sasa,sijui nichukue hatua gani baada ya kukasirishwa na TAKUKURU...
   
 2. NDAMANDOO

  NDAMANDOO JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 250
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 45
  PCCB hawana lolote hao kazi yao kubwa ni kuwahoji watoa rushwa ndogondogo kama vile ya driver daladala kumpa traffic police elfu mbili.......... kuna haja ya kuivunja na kuunda tume huru ya kupambana na kuzibithi rushwa. lakini pia sheria itoe muongozo kuhusu ipi rushwa ya TA--KUKU--RU na ipi TAKUKURU.
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Wakili kichwa na maelezo yako mie mh!
   
 4. Mundali

  Mundali JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2012
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 749
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  TA - Taasisi ya
  KU - Kuboresha na
  KU - Kustawisha
  RU - Rushwa Tanzania.
   
 5. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,550
  Likes Received: 4,675
  Trophy Points: 280
  Mkuu si unakumbuka yale ya Richmond? Takukuru ni sabuni ya kuwasafisha viongozi wanaokabiliwa na tuhuma za rushwa.
   
 6. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 548
  Trophy Points: 280
  Hivi kwa mujibu wa profession ya sheria, si haitakiwi kutoa siri za mteja wako?
   
 7. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hii ndio Bongo bana. Labda ungemchunguza vizuri huyo Afisa ungeweza kukuta huenda nae ni miongoni mwa wale Wanaoendelea kufichuliwa na NIDA ( Wakala wa Vitambulisho vya Uraia). Atakuwa nae anatumia jina la Marehemu kaka yake hapo.
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Naona wamechelewa sana! Watanzania wengi walitarajia kuisiki hii TAKUKURU ikiwasafisha siku ile ile ya mjadala bungeni!
   
 9. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,068
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  kwahiyo unataka kusema mkullo ni mteja wake?
   
 10. M

  Mgosingwa Member

  #10
  May 21, 2012
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri umefika wakati sasa watanzania tuamue kupitia bunge letu kuifuta Taasisi hii ambayo haina faida yoyote kwa Mtanzania zaidi ya kutuongezea gharama tu, tukiangalia tangu ilipoanzishwa rushwa imeendelea kuongezeka tu na imekuwa ndiyo kichaka cha wala rushwa wakubwa.
   
 11. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Siri ni ipi hapo? Kusema mteja wake anatuhumiwa kupokea rushwa ya laki tatu ni siri nayo? Mahakamani kesi hiyo inatajwa vipi?
   
 12. j

  jovitha mussa Member

  #12
  May 21, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  Natafuta nchi ya kuhami
   
 13. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Takukuru ni toothless dog
   
 14. Jumboplate

  Jumboplate Senior Member

  #14
  May 21, 2012
  Joined: Jul 29, 2008
  Messages: 133
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyo afisa wa takukuru atakuwa alikuona we kichwa maji! Sasa hayo ni maswali ya kumuuliza mchunguzi halafu akujibu kirahisi tu?
   
 15. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #15
  May 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,814
  Trophy Points: 280
  Mkuu kumbe wewe mwanasheria!! Piganeni tupate private investigators and prosecutors. Hayo yote yataisha
   
 16. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  alaahh kumbe TAKUKURU wao wanasubiri amri kutoka kwa wakuu wao?? nilifikiri wanachunguza kesi kutokana na ushahidi walionao....SI MCHEZO...IT CAN ONLY HAPPEN IN BONGO
   
 17. M

  MTK JF-Expert Member

  #17
  May 21, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Hivi wewe umesahau threads za Julian Assange na weakleaks yake kuhusu "Kideri" cha Takukuru ?!
   
 18. s

  sexon2000 JF-Expert Member

  #18
  May 21, 2012
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 300
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  It is not a dog at all, may be a goat!!!!
   
 19. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #19
  May 21, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi kuna mtu aliamini kuwa takukuru kweli inawachunguza akina Mkulo? Yangekuwa ni maajabu ya nane ya dunia
   
 20. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #20
  May 21, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mbwa huwa hamng'ati boss wake
   
Loading...