Takukuru kuchunguza fedha chafu za kuwang`oa wabunge

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,816
678
Takukuru, mmefanya la maana sana; tena anzieni Kyela.

Takukuru kuchunguza fedha chafu za kuwang`oa wabunge
Na Thobias Mwanakatwe



29th December 2009




headline_bullet.jpg
Ni mamilioni wanayomwaga mafisadi majimboni
headline_bullet.jpg
Yasema imeanza kuchunguza madai kabla ya hatua
headline_bullet.jpg
Yaeleza wabunge ni watu wenye heshima kwa jamii



Mwambalaswa(1).jpg

Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa



Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) Mkoa wa Mbeya imetangaza kuanza rasmi mchakato wa kufanya uchunguzi wa kina kufuatia madai ya kuwepo kwa watu ambao wanasambaza fedha kwenye majimbo ya mkoa huo kwa ajili ya kuwang'oa baadhi ya wabunge wa sasa katika uchaguzi mkuu ujao.

Hatua ya Takukuru kutangaza kuanza uchunguzi huo, inafuatia malalamiko kadhaa yanayoendelea kutolewa na wabunge kadhaa wa Mkoa Mbeya kwamba mtandao wa mafisadi unasambaza mamilioni ya fedha chafu kwenye majimbo yao kwa ajili ya kuhakikisha wabunge wapambanaji wa ufisadi hawachaguliwi katika Uchaguzi Mkuu wa mwakani.

Wabunge ambao hadi sasa wameshatangaza bayana kuwa mafisadi wamesambaza fedha kwenye majimbo yao ni Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa, Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe na Mbunge wa Mbeya Mjini, Benson Mpesya.

Kwa mujibu wa wabunge hao, fedha hizo zinasambazwa majimboni na mawakala wa mafisadi pamoja na watu ambao wanakusudia kugombea ubunge mwakani ambao inadaiwa wamefadhiliwa na mafisadi ili kuwang'oa madarakani wabunge wa sasa.

Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Mbeya, Resticks Ndowo, akizungumza jana na Nipashe, alisema taasisi yake imeanza kuyafanyia uchunguzi madai ya wabunge ili kubaini ukweli wake na kuchukua hatua zinazostahili.

''Wabunge ni watu wenye heshima katika jamii kwa hiyo hatuwezi hata kidogo kupuuza malalamiko yao, tutayafanyia uchunguzi na kuchukua hatua zinazostahili kwa wahusika kama watabainika,'' alisema Ndowo.

Hata hivyo, Ndowo alisema kuwa ili kazi yao hiyo iweze kufanikiwa wabunge hao watoe ushirikiano kwa Takukuru kwa kutoa ushahidi utakaowezesha kutiwa mbaroni kwa watu wanaosambaza fedha hizo.
Majimbo ya uchaguzi ya Mkoa wa Mbeya mengi wamejitokeza watu wengi wanaotaka kugombea ubunge mwakani kupambana na wabunge wa sasa kutokana na imani waliyojiwekea kuwa wabunge wengi wa sasa hawatapitishwa na vikao vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa sababu wapo mstari wa mbele kufichua na kukemea vitendo vya ufisadi.

Tangu Dk. Mwakyembe alipowasilisha bungeni ripoti ya Kamati ya Uchunguzi ya Bunge iliyochunguza zabuni tata ya kufua umeme wa dharura iliyoipa ushindi Kampuni ya Richmond LLC ya Marekani, amekuwa akilalamika kuwa kuna kundi la mafisadi linalomwaga fedha katika jimbo lake ili kuhakikisha anaangushwa mwakani.
Mbunge huyo aliwasilisha ripoti ya Richmond Februari 6, mwaka jana ikibainisha kuwa Richmond ilikuwa kampuni ya mfukoni na kwamba haikuwa na uwezo wa kuzalisha umeme.

Kuwasilishwa kwa ripoti hiyo kuliwalazimisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, na mawaziri wawili walioiongoza Wizara ya Nishati na Madini kwa nyakati tofauti Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi siku moja baadaye Februari 7, 2008 kujiuzulu kutokana na kuguswa na kashafa hiyo.

Wiki iliyopita, Mpesya alisema kuwa pamoja na mafisadi kutenga mamilioni ya fedha kwa ajili ya kuwashughulikia wabunge wanaopambana na ufisadi, yuko tayari kunyang’anywa ubunge huo katika Uchaguzi Mkuu mwakani, lakini kamwe hatawaunga mkono wala kuwatetea mafisadi.

Mpesya alisema akiwaunga mkono mafisadi atakuwa anawasaliti Watanzania na kwamba msimamo wake wa kutowaunga mkono mafisadi unatokana na ukweli kwamba ubunge ni heshima ya kupewa na wananchi hivyo hawezi kusema yeye ni bora kuliko wananchi waliomchagua ambao wanauchukia ufisadi kwa kuwa wanatambua kuwa unaitafuna nchi na kuwasababishia waendelee kuwa maskini.
Alidai kuwa watu wanaotuhumiwa kwa ufisadi wametengeneza mtandao na wametenga mamilioni ya fedha kwenye majimbo kwa ajili ya kuwashughulikia wabunge wanaopambana na ufisadi lakini yeye (Mpesya) hatishiki na mpango huo na yupo tayari kuupoteza ubunge lakini kamwe hataweza kuwaunga mkono mafisadi.

Akizungumza mbele ya Dk. Mwakyembe na Mbunge wa Rungwe Mashariki, Profesa Mark Mwandosya katika hafla ya uzinduzi wa Chama Cha Wafanyabiashara mjini Mbeya, Mpesya alidai kuwa fedha hizo chafu zilizotengwa kuwamaliza wabunge wapambanaji wa ufisadi zitasambazwa na mawakala wa mafisadi ambao wapo kila mkoa na kila jimbo.

Naye Mwambalaswa, alidai juzi kuwa mtandao wa mafisadi umeji penyeza jimboni mwake kwa kusambaza fedha chafu zaidi ya Sh. milioni 60 kwa lengo la kutaka kumung'oa madarakani mwakani.
Mbunge huyo alitoa madai hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Mbeya, kuelezea mambo aliyokutana nayo wakati yupo kwenye ziara ya kutembelea wapiga kura wake.
Alisema katika ziara yake alibaini kuwa fedha hizo zimesambazwa katika vijiji vya jimbo la Lupa kwa lengo la kushawishi wananchi wasimchague.

Kwa mujibu wa Mwambalaswa, fedha hizo ambazo ana imani zimetolewa na mtandao wa mafisadi, zinasambazwa na mawakala wa mafisadi, wakiwemo watu wanaotaka kugombea ubunge jimboni humo mwakani.

Mwambalaswa alisema kutokana na fedha hizo kugawiwa ovyo vijijini, wananchi wameingiwa na hofu kubwa na kuhoji kama watu hao wanaozisambaza wana lengo zuri kwenye jimbo hilo kwani iwapo watakosa ubunge nini hatma kwa wananchi watakaokuwa wamepewa mamilioni hayo.

Mbunge huyo ambaye hakutaka kuweka uwazi katika suala hilo, alisema fedha hizo chafu zimeletwa katika jimbo la Lupa kutoka kampuni moja ya ujenzi iliyopo mkoani Mwanza na kwamba uthibitisho wa kusambazwa kwa mamilioni hayo ameupata kutoka kwa wananchi ambao wamegawiwa.

Mwambalaswa alisema hata hivyo, anashangaa mafisadi kusambaza fedha hizo wakati yeye (Mwambalaswa) hajawahi kuwashambulia mafisadi hata siku moja.
Alisema hata hivyo, hatishiki na mafisadi kumwaga fedha hizo na kuwataka wananchi kukaa mkao wa kula mamilioni hayo ila wajiulize wanaotoa fedha hizo wanania gani na je, wasipochagulia hatma yao itakuwa nini.
 
Du mafisadi wanatuwahi kila sehemu: Wanajaribu kutu pre empty on every move! Hivi kweli Takukuru inayoongozwa na fisadi Hosea inaweza kuwachunguza mafisadi wenzie waliotoa milioni 400? kaputi
 
Nasubiri kuona Takukuru wakisafiri hadi uingereza (kwa gharama za nani sijui) ili kupanua wigo wa uchunguzi wao.
 
TAKUKURU kwenyewe kumejaa mafisadi kibao ndiyo maana hadi hii leo hawajakamilisha uchunguzi wowote wanaacha hili wanarukia lile. UPUUZI MTUPU!
 
Takukuru waanze kujichunguza kwanza wao ndipo wafuate wengine.Je wao ni wasafi kwa kiwango gani?mimi sina imani kabisa na Takukuru.
 
Back
Top Bottom