Takribani miaka 20 ya elimu shuleni imezidiwa na miaka miwili ya mafunzo mtaani

BUSARA ZANGU

JF-Expert Member
May 5, 2013
779
1,267
Habari ya weekend

Katika maisha yangu na pengine wengi wetu humu, tumetumia muda wetu mwingi kupata Elimu ya darasani japo mengi tuliyojifunza hayakidhi matakwa ya mahitaji ya mtaani. Kiujumla tunaenda shule ili tuje tupate sifa zitakazotusaidia kupata ajira, ili hiyo ajira itupatie kipato/pesa.

Darasani hatufundishwi kuja kugundua fursa, kuja kugundua vipaji wala hatufundishwi kuja kuwa watengenezaji wa ajira. Hatufundishwi kutengeneza pesa, jambo ambalo ni msingi mkubwa Elimu tunapewa ili tuje tupate ajira. Darasani tunafundishwa jinsi Elimu ilivyo mtaji namna tunavyopaswa kuwa wavumilivu tukiwa kazini na kwamba ipo siku wakubwa huko juu watatuona na kutupatia kacheo kanachoendana na shule yetu.

Huwa najiuliza kwanini kwenye mitaala hawataki kujumuisha Elimu ya ujasiriamali kuanzia chini shule za msingi mpaka kwenye vyuo? Kwanini hamna Elimu ya pesa, wakati pesa ndio kila kitu kwenye haya maisha ya kidunia? Pesa ni nini, njia za kupata pesa, njia kutunza pesa, njia za kuongeza pesa, Maeneo ya kuwekeza pesa n.k. Kwangu mimi nnaona haya ni maeneo ya muhimu sana ya kuzingatia kwenye Elimu yetu.

Nikiwa mkweli, Elimu ya miaka ishirini niliyoipata imenipa mambo 3 tu makubwa, ambayo ni 'k' 3, KUSOMA, KUANDIKA NA KUHESABU na haya mambo niliyoipata miaka miwili mitatu ya mwanzoni nilipokuwa shule, yaliyobaki mengine nisingejuta kuyakosa endapo ningeyakosa.

Kuna mambo ambayo nimejifunza katika hii miaka miwili ambayo Nadhani ni zaidi ya yale niliyofundishwa Darasani kwa takribani miaka 20.

1. Dhamira ni kila kitu

Dhamira inafanya yasiyowezekana kuwezekana, Dhamira inahamisha milima. Dhamira ilimfanya Edison kugundua taa ya bulb mara baada ya majaribio yake ya awali takribani 10, 000 kushindwa. Dhamira ilimfanya Colonel Sander kupata utajiri wake akiwa na miaka zaidi ya 60 mara baada ya kufilisika hapo awali.

2. Fanya maamuzi

Siku zote mipango bila utekelezaji inabaki kuwa ndoto. Umewaza kufanya jambo? Fanya leo, usisubiri kesho.

3. Mwanzo mgumu, mbele kwepesi

Kutengeneza pesa ni kama kujifunza kuendesha baskeli. Utakapoanza, utashikiwa baskeli, utaanguka, utaanza kuendesha kwa kutanga njia nzima kisha utakuwa fundi. Ndivyo ilivyo kwenye kutafuta pesa, mwanzo ni mgumu sana (ni kama foundation stage), once you take off... No body will be capable to catch you.

4. Dhibiti maadui wa Utajiri

Wakati uingereza wapo kwenye hatua ya mapinduzi ya kilimo kuelekea kwenye mapinduzi ya kisayansi na kiviwanda kuna mwandishi mmoja alitaja maadui 3 wa maendeleo ambao ni uvumbuzi, wanawake na pombe. Mimi leo nakwambia kaa mbali na maadui hao wawili wa mwisho na kamari ambayo inaweza kuwa tafsiri ya starehe.

5. Fanya kazi, ingiza kipato, weka akiba, wekeza akiba, wekeza faida ya akiba uliyowekeza

Kufanya kazi pekee yake, kuweka akiba na kuwekeza akiba pekee haitoshi. Kama unampango wa kufika mbali kimaisha, always wekeza faida ya akiba uliyowekeza.

6. Fanya jambo tofauti, sio jambo unalolipenda

Kuna upotoshaji kwamba ili mtu ufanye vizuri kwenye maisha wekeza kwenye jambo unalolipenda. Ki ukweli hata kama unapenda soka vipi, huwezi lazimisha kucheza ufike level za professional kama kipaji ni cha kuunga Unga. Ama tuseme wewe unapenda mambo ya gymnastic lakini upo vijijini utaanzisha gym? Nani atakuwa mteja wako?

7. Ishi kwa kufuata bajeti

Hili ni tatizo letu wengi sana. Tunafanya manunuzi kwa chochote tunachokutana nacho mbele bila kujali kama kipo kwenye mipango yetu ama laa. Nimejifunza bajeti ni msingi wa kutopoteza fedha hovyo hovyo.

8. Weka akiba, weka akiba, weka ajiba

Hapo awali nilikuwa naweka akiba kile kilichobaki baada ya kufanya matumizi, badala ya kuweka akiba kisha kinachobaki ndio nifanye matumizi. Huu ni ugonjwa wa wengi sana.

9. Always kuwa na fedha inayoonekana kama haina kazi kwenye akaunti yako

Kuna nyumba moja yenye thamani ya Tsh milioni 80+ imeuzwa kwa Tsh milioni 42 tena mnunuaji hakulipa fedha zote kwa mkupuo. Kiufupi hiyo nyumba Ilikuwa inamuingizia mwenye nyumba almost 1,000,000/= kwa mwezi. Nimeona viwanja na mali nyingi watu wamejichukulia kwa kuwa wamekuwa na akiba kwenye akaunti zao.

10. Nunua mali zinazozalisha mali (Income generating assets)

Gari za kutembelea, nyumba za kuishi, mikufu ya dhahabu n.k havitakusaidia kwenye maisha yako. Nunua/jenga nyumba za kupangisha, mashamba, viwanja n.k ili uongeze kipato chako. Matajiri wengi wamekuwa wakitumia hii mbinu.

11. Sehemu salama ya kuwekeza ni kwenye majengo na ardhi

Matajiri wote unaowafahamu wanamiliki makampuni mbali mbali lakini ukiwauliza wewe hasa umewekeza kwenye nini atakwambia ni kwenye Real Estates. Tafuta pesa, wekeza kwenye real Estates. Ieleweke kwamba hata hii biashara inachangamoto zake, lakini still is the best bet.

12. Hakuna njia ya mkato ya kupata pesa

Mimi ni moja kati ya wahanga wa njia za mkato. Mpaka sasa DECI wana kama laki 5 zangu ambazo nimeshazisamehe maana najua serikali ilishazitumia. Kwasasa naona kuna DECI nyingi katika maumbo mbali mbali zikishamiri. Njia za mkato ni hatari kwa pato lako.

13. Hakuna mwajiriwa tajiri
Kama unataka kuwa Tajiri, jiajiri. Kama unataka kuwa average/middle class au masikini ajiriwa. Na kila siku sheria za Mashirika ya kijamii kuhusu pension zetu zinabadilishwa, kwahiyo kwa waajiriwa, kufa masikini is guaranteed.

14. Kuwa na Mtazamo wa mbali

Kama unataka kufanikiwa kimaisha, kwenye angle ya kiuchumi basi kuwa na huu mtazamo. Wanaita long term view. Mfano nunua kipande cha ardhi ukiwaza sio lazima kininufaishe leo, hata miaka 5 au 10 kitaninufaisha. Nunua hisa, Nunua nyumba, panda miti, tafuta marafiki/jenga mtandao n.k ukiwa na huu mtazamo. Trust me, it pays.

15. Jengo nyumba/fanya Miradi mkubwa ukiwa tayari

Unaweza imagine umepoteza Tsh ngapi kwenye ujenzi wa nyumba yako? Nyumba umeijenga kwa milioni 30 kwa miaka 10 na haijaisha, ina maana hiyo milioni 30 ipo chini ya ardhi kwa miaka 10 bila hata kukuingizia hata elfu tano. Kwa rate ya fixed akaunti (18% kwa mwaka) hiyo milioni 30 kwa miaka 10 ingekuingizia Tsh milioni 54 zaidi. Hapo ungewekeza kwenye jambo lingine pengine ungeingiza za ya hiyo milioni 54.

Mwisho:elimu ina umuhimu wake lakini Elimu ya pesa ina umuhimu zaidi. Hapa nilipo ninaandaa mtaala kwa ajili ya elimu ya pesa kwa wanangu. Nawatakia sherehe njema za Christmas na kuuaga na kuukaribisha mwaka Mpya.
 
Nice article.

Ila maswala ya kusema Gari ya kutembelea haitakusaidia kwny maisha ni uongo mtupu.Wengine deals huku mtaani tunazipata sababu ya Kuaminiwa na watu kutokana na Gari tunazoendesha.
Mkuu umenena vizuri. Je kwa matumizi hayo uliyoyataja (ya kujenga trust ili upate dili), hiyo gari itabaki kuwa gari ya kutembelea?
 
Labda sijaelewa swali vzr mkuu wangu.
Hoja ni kwamba kuna wakati mark 2 inaweza kuwa mzigo,pale unapoitumia kupigia misele na kufuatilia mademu, lakini pengine ukiitumia kwenye tax itakuingizia kipato na badala ya mzigo itakuwa msaada kwako.

Ni sawa na wewe ulivyosema kwamba unatumia gari yako kukuingizia mkwanja badala kukutia hasara. So hiyo gari kwako si kutembelea tena bali ni gari ya kazi, ya kukupa madili.
 
Hoja ni kwamba kuna wakati mark 2 inaweza kuwa mzigo,pale unapoitumia kupigia misele na kufuatilia mademu, lakini pengine ukiitumia kwenye tax itakuingizia kipato na badala ya mzigo itakuwa msaada kwako.

Ni sawa na wewe ulivyosema kwamba unatumia gari yako kukuingizia mkwanja badala kukutia hasara. So hiyo gari kwako si kutembelea tena bali ni gari ya kazi, ya kukupa madili.
Sawa mkuu nimekuelewa,tuko pamoja.

Kudos.
 
Miundo mbinu mibovu pamoja na Uongozi usiojali na kuthamini vipaumbele vya Wananchi wake, ni chanzo kikuu (kikubwa) cha Umasikini Nchini...!
 
Miundo mbinu mibovu pamoja na Uongozi usiojali na kuthamini vipaumbele vya Wananchi wake, ni chanzo kikuu (kikubwa) cha Umasikini Nchini...!
Chanzo kikuu cha umaskini kipo katika fikra. Unajua katika mazingira hayo hayo unayoyasema kuna watu walikuwa maskini ila miaka mitatu baadaye walikuja kuwa watu tofauti? Na kuna wengine wapo kwenye maisha duni leo ila baada ya miaka 2 watakuwa watu tofauti?
 
Back
Top Bottom