Takriban raia 132 wa Tanzania wanaoishi nchini Msumbiji wamefurushwa nchini humo

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,411
Takriban raia 132 wa Tanzania wanaoishi nchini Msumbiji wamefurushwa nchini humo huku wengine wasiojulikana wakidaiwa kukamatwa kufuatia operesheni ilioanzishwa na serikali ya taifa hilo.

Kulingana na serikali ya Msumbiji operesheni hiyo inalenga kuwatimua raia wa kigeni wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki nchini Tanzania imesema kuwa raia waliofukuzwa ama hata kukamatwa ni wale wanaoishi mji wa Monte Puez kwa kuwa una raia wengi wa kigeni ikilinganishwa na miji mingine.

Kulingana na taarifa hiyo tayari ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji unaendelea kufanya mawasiliano ya kidiplomasia na serikali ya Msumbiji ili kuwahakikishia usalama raia wa Tanzania na mali yao nchini humo.

Inakadiriwa kuwa, Watanzania wapatao elfu tatu (3,000) wanaishi na kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii katika mji huo wa Monte Puez.

Hatua hiyo inajiri licha ya mataifa ya Msumbiji na Tanzania kufanya mkutano wa kuainisha maeneo ya ushirikiano yakiwemo maswala ya kibiashara na uhamiaji.

Na huku operesheni hiyo ikiendelea serikali ya Tanzania imekuwakumbusha Watanzania wote waishio ughaibuni, kufuata Sheria na taratibu za nchi hizo wanazoishi.

Chanzo: BBC/Swahili
 
Raia wa Tz hawana samani
Hakuna chochote hapo
Na hakuna kiongozi anaesikia uchungu
Juu ya watz wanaoua nje ya nchi
Ni wengi walisha uawa lakini hakuna kitu

"Ni aibu raia wa nchi hii kuuliwa nje huko"
Na pasipo hatua yoyote kuchukuliwa.
Ficha upumbavu wako
Huu ni uchochezi usio na maana
 
Tobaa..! hapa panahitaji hekima mkuru na kauli zileeee.. hapo si mahala pake
 
Kuna taarifa tangu jana zilikuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii, kuhusu watanzania waishio Msumbiji wamekamatwa na serikali ya huko na kuuwawa!ikiwa ni pamoja kuwekwa jela kwa kilichoelezwa kuwa waondoke Msumbiji sikwao!! na hata kama ulikuwa na karatasi halali za kuishi huko na kufanya kazi wametiwa ndani pia ,na hawakuwa na mda wakusoma dokment za mtu yoyote!! hata pasi za kusafiria zimechomwa!! hadi jana watu walikuwa hawatoki ndani!!!Inasadikika watu 4 walipoteza uhai!.Na hilo katika kipindi cha PowerBreakfast cha Clouds amesikika mtu akiojiwa na Clouds kuhusu hali ya huko na alikuwa akiomba msaada.
Hivyo tunaomba serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ichunguze hizi tuhuma.
Mkuu alitamka kama watakuwa wamekutwa na hatia kama ya madawa ya kulevya na kuhukumiwa kunyongwa acha wanyongwe,
 
Kuna taarifa tangu jana zilikuwa zikisambaa katika mitandao ya kijamii, kuhusu watanzania waishio Msumbiji wamekamatwa na serikali ya huko na kuuwawa!ikiwa ni pamoja kuwekwa jela kwa kilichoelezwa kuwa waondoke Msumbiji sikwao!! na hata kama ulikuwa na karatasi halali za kuishi huko na kufanya kazi wametiwa ndani pia ,na hawakuwa na mda wakusoma dokment za mtu yoyote!! hata pasi za kusafiria zimechomwa!! hadi jana watu walikuwa hawatoki ndani!!!Inasadikika watu 4 walipoteza uhai!.Na hilo katika kipindi cha PowerBreakfast cha Clouds amesikika mtu akiojiwa na Clouds kuhusu hali ya huko na alikuwa akiomba msaada.
Hivyo tunaomba serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje ichunguze hizi tuhuma.

Mimi hata huwa najiuliza kwa nini tulipoteza askari wetu kwenda kupigania uhuru wa Msumbiji majitu yasiyo na shukrani yenye mioyo ya kishetani kabisa.

Haya majitu siku zote hayakumbuki fadhila. Watz Wengi wamekuwa wakilalamika kufanyiwa unyama wa kutisha ikiweno kunyang'anywa mali zao, kuuawa, uchomewa nyaraka na kubambikizwa kesi na hawapewi nafasi y akujitetea.

Naunga mkono hoja. Bwana Mahiga, Watz, wanauawa msumbiji,naomba muonyeshe kuwajali hawa ni raia wetu. Serikali haina kazi y akupambana na wapinzani wala wakosoaji wake tu.
 
Takriban raia 132 wa Tanzania wanaoishi nchini Msumbiji wamefurushwa nchini humo huku wengine wasiojulikana wakidaiwa kukamatwa kufuatia operesheni ilioanzishwa na serikali ya taifa hilo.

Kulingana na serikali ya Msumbiji operesheni hiyo inalenga kuwatimua raia wa kigeni wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki nchini Tanzania imesema kuwa raia waliofukuzwa ama hata kukamatwa ni wale wanaoishi mji wa Monte Puez kwa kuwa una raia wengi wa kigeni ikilinganishwa na miji mingine.

Kulingana na taarifa hiyo tayari ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji unaendelea kufanya mawasiliano ya kidiplomasia na serikali ya Msumbiji ili kuwahakikishia usalama raia wa Tanzania na mali yao nchini humo.

Inakadiriwa kuwa, Watanzania wapatao elfu tatu (3,000) wanaishi na kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii katika mji huo wa Monte Puez.

Hatua hiyo inajiri licha ya mataifa ya Msumbiji na Tanzania kufanya mkutano wa kuainisha maeneo ya ushirikiano yakiwemo maswala ya kibiashara na uhamiaji.

Na huku operesheni hiyo ikiendelea serikali ya Tanzania imekuwakumbusha Watanzania wote waishio ughaibuni, kufuata Sheria na taratibu za nchi hizo wanazoishi.

Chanzo: BBC/Swahili
Kuna FURSA nyingi sana huko hasa za uchimbaji wa madini ya Ruby. Wenyeji ni wavivu na mwanzoni walikuwa hawafuatilii kazi hizi. Warudi kwanza nyumbani halafu wafuate utaratibu na diplomats wafanye kazi hii kwa pamoja. Wenyeji wanawahitaji sana watanzania.
 
Takriban raia 132 wa Tanzania wanaoishi nchini Msumbiji wamefurushwa nchini humo huku wengine wasiojulikana wakidaiwa kukamatwa kufuatia operesheni ilioanzishwa na serikali ya taifa hilo.

Kulingana na serikali ya Msumbiji operesheni hiyo inalenga kuwatimua raia wa kigeni wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.

Taarifa ya wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki nchini Tanzania imesema kuwa raia waliofukuzwa ama hata kukamatwa ni wale wanaoishi mji wa Monte Puez kwa kuwa una raia wengi wa kigeni ikilinganishwa na miji mingine.

Kulingana na taarifa hiyo tayari ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji unaendelea kufanya mawasiliano ya kidiplomasia na serikali ya Msumbiji ili kuwahakikishia usalama raia wa Tanzania na mali yao nchini humo.

Inakadiriwa kuwa, Watanzania wapatao elfu tatu (3,000) wanaishi na kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii katika mji huo wa Monte Puez.

Hatua hiyo inajiri licha ya mataifa ya Msumbiji na Tanzania kufanya mkutano wa kuainisha maeneo ya ushirikiano yakiwemo maswala ya kibiashara na uhamiaji.

Na huku operesheni hiyo ikiendelea serikali ya Tanzania imekuwakumbusha Watanzania wote waishio ughaibuni, kufuata Sheria na taratibu za nchi hizo wanazoishi.

Chanzo: BBC/Swahili
Watu wanamchukia bure Trump
 
Huyo anae bisha ni mpumbavu na taahira wa akiri huku ni noma yaani zaidi ya noma na wote waishio katika wilaya ya montipuez wamepewa siku tano tu kuondoka hailishi una mali hauna wewe toka tu
 
Back
Top Bottom