PaulMasatu.com
Member
- Oct 10, 2014
- 6
- 4
Dont test the depth of water with both feet -Warren Buffett
Kuelekea kwenye kutimiza ndoto yako, kuna jambo moja muhimu la kujifunza, nalo ni ku take risk, na siyo tu just a risk, inatakiwa iwe calculated risk!
Kila kitu kwenye maisha kina involve risk, hakuna kitu ambacho ni salama kwa asilimia mia moja, ngoja nikupe mifano
- Usafiri tunao utumia kuja makazini kila siku una kiwango cha risk, chochote chaweza kutokea na kugharimu maisha yetu
- Chakula tunachokula kina kiwango cha risk
Nini maana yak u take risk?
Taking risks mean stepping out of what is safe, comfortable and familiar to you. Ni ile hali ya kuondoka katika hali yako ya kawaida uliyo izoea na kuishinda hofu kwa kuchukua hatua za kijasiri zaidi kuelekea kutimiza ndoto zako, siyo swala jepesi kufanya, kwasababu linagusa hisia zako, na mara nyingi hisia inayo husika hapa ambayo inabidi uishinde ni hofu, hofu ya kushindwa, hofu ya kupoteza n.k lakini kama nilivyo kueleza hapo juu, usiogope ku take risk, unachotakiwa kufanya ni ku take a calculated risk.
Zipo hatua kadhaa unaweza kuzifanya ambazo zitakuwezesha ku calculate risk kwenye kila hatua unayotaka kuchukua,kwenye makala hii nitakueleza hatua moja tu, ukitaka kujua hatua nyingine endelea kunifuatilia, nikiweka mkazo zaidi kwenye eneo la uwekezaji ambalo litakupa ongezeko la kipato na kukuwezesha kutimiza ndoto zako.
1. Wekeza kwenye maarifa( Invest in education).
There is no bad investment, only bad investor Robert Kiyosaki
Sentensi hiyo hapo juu ya kutoka kwa bwana Robert Kiyosaki, inaonyesha kwa uwazi kabisa tatizo liko wapi, watu wengi hawataki kuwekeza kwenye maarifa, matokeo yake inapofika muda wa kuchukua hatua, iwe kwenye uwekezaji au jambo lingine lolote wanakwenda blindly tu kwa kufuata mkumbo wa watu wengine wanafanya nini, matokeo yake wanapata hasara ya kupoteza muda na fedha zao, hii experience inawajengea hofu ndani yao, matokeo yake na inapotokea nafasi ambayo wanatakiwa wachukue hatua ili kutimiza ndoto zao utawasikia, this is so risky and I know this is not for me. Tumia muda na fedha zako, tafuta maarifa, sikiliza DVDs za mafundisho, huzuria semina, nunua vitabu na machapisho mbalimbali, tafuta mtu(mentor) ambaye mwenye ujuzi na maarifa ambaye ameshapita huko unapotaka kupita, jifunze kutoka kwake, hii itakujengea uwezo, na utakapo chukua hatua, zitakuwa ni hatua zenye calculated risk.