Taiwan kununua Makombora ya HIMARS

Axel Lloyd

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
4,169
9,499
Taiwan imetenga fedha kwenye bajeti yake ya Ulinzi mwaka huu kununua Makombora ya HIMARS (29 launchers pamoja na maroketi 864) pia Makombora yake mazito ya ATACMS yenye uwezo kupiga adui umbali wa Hadi 300km.

Haya yanajiri baada ya Taiwan kuongeza bajeti yake ya jeshi kwa asilimia 14 kutokana na vitisho vya China.

Taiwan ilipanga kununua mizinga ya M109A6 "Paladin" lakini kutokana na mafanikio ya HIMARS dhidi ya vikosi vya Urusi imesitisha dili hilo ambalo lilishaidhinishwa na utawala wa Biden na sasa itanunua Makombora ya HIMARS.

Poland pia imeweka oda ya kununua Makombora 500 ya Himars. Estonia,Lithuania pia zimeweka oda ili kupata mizinga hiyo.

Taiwan eyes HIMARS rockets for defense against China
 
Hili dude linaitwa kuzimu ,limeua sana huko Ukraine, Putin hatak hata kulisikia ,wanajeshi wa Russia wakilisikia miguu yote inatepeta,S400,S300 zote zimegonga mwamba kulizuia ili limzimu
 
... halafu katika stock ya silaha ya US, HIMARS ni very inferior! Akitoa zile zenyewe achana na nukes masupa pawa wa michongo watatafutana. Wale wanaofanyaga magwaride ya silaha mitaani kila mwaka.
 
Kama namuona Putin anavyonuna akiiyaona haya madude.
Sijui anajisikiaje na ule mkwara wake wa atakayeingilia operesheni atakiona Cha moto

Madude hayakosei haya
 
... halafu katika stock ya silaha ya US, HIMARS ni very inferior! Akitoa zile zenyewe achana na nukes masupa pawa wa michongo watatafutana. Wale wanaofanyaga magwaride ya silaha mitaani kila mwaka.
Hii kitu ya zamani sana imefanya kazi Gulf war ila leo ndo champion against super pawa
 
Hawa jamaa Taiwan tunaaminishwa ndio wabobezi wa technology.. Na USA anawang'ang'ania Kwaajili hiyo.
Sasa inakuaje wanashindwa kujiendesha wao wenyewe? Inakuaje tena wananunua hayo makombora kutoka USA!
 
... technology ziko za maeneo mengi mzee; from ICT to medical; from weapons to astronomy; from artificial intelligence to marine; etc. Taiwan haijawekeza sana kwenye weapons compared to US, China, and Russia; ila ni kati ya jamii zenye watu wenye akili nyingi sana duniani mixture of Japanese, Koreans, Chinese, Filipinos, et.al. inatoa brains fulani za hatari.
 
Taiwan imetenga fedha kwenye bajeti yake ya Ulinzi mwaka huu kununua Makombora ya HIMARS (29 launchers pamoja na maroketi 864) pia Makombora yake mazito ya ATACMS yenye uwezo kupiga adui umbali wa Hadi 300km.

Haya yanajiri baada ya Taiwan kuongeza bajeti yake ya jeshi kwa asilimia 14 kutokana na vitisho vya China.

Taiwan ilipanga kununua mizinga ya M109A6 "Paladin" lakini kutokana na mafanikio ya HIMARS dhidi ya vikosi vya Urusi imesitisha dili hilo ambalo lilishaidhinishwa na utawala wa Biden na sasa itanunua Makombora ya HIMARS.

Poland pia imeweka oda ya kununua Makombora 500 ya Himars. Estonia,Lithuania pia zimeweka oda ili kupata mizinga hiyo.

Taiwan eyes HIMARS rockets for defense against China
Hayo makombora si chochote si lolote kama urusi ikitum8a makombora ya kusambaratisha satelite
 
... halafu katika stock ya silaha ya US, HIMARS ni very inferior! Akitoa zile zenyewe achana na nukes masupa pawa wa michongo watatafutana. Wale wanaofanyaga magwaride ya silaha mitaani kila mwaka.
Russia aijatumia silaha zakw kubwa kama za kuripua satelite ambazo ndoyo moyo wa silaha za USAkama hizo HIMARS
 
Hii kitu ya zamani sana imefanya kazi Gulf war ila leo ndo champion against super pawa
Unajua kuwa moyo wa HIMARS NI SATELITE? SASA MRUSI AJATAKA TU KUKUZA VITA DAWA NI KUPIGA HIZO SATELITE TU NDIYO MAANA USA ANAMYOGOPA MRUSI
 
Kama urusi angekuwa na uwezo wa kufanya hivyo Wala hasingechelewa kuzilipua hizo satellite

Hiyo midude inaua asikari wake kama kumbikumbi,na kuteketeza maghala kibao., Halafu urusi aone kabisa kuwa Kuna uwezekano wa kufanya jambo juu kudhibiti madude haya asubiri?

Nitakuwa wa mwisho kuamini hizi hekaya
Kwahiyo wewe unadhani urusi hana huo uwezo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom