Taifa stars ya miaka 50 ya uhuru

MzeePunch

JF-Expert Member
Jun 8, 2009
1,412
203
Hebu tuchangie mawazo kupata timu ya wachezaji bora wa mpira wa miguu waliowahi kuchezea Taifa Stars katika kipindi cha miaka 50 iliyopita. Wale waliowashuhudia wachezaji wa miaka ya mwanzoni mwa 60 watatusaidia iwapo wanawakumbuka ma-star wa enzi hizo waliokuwa na kipaji adimu cha kutandaza kabumbu. Kikosi kijumuishe wachezaji wa 1961 - 2011. Binafsi nilivutiwa sana na uchezaji wa hawa wafuatao ambao niliwahi kuwashuhudia uwanjani na ninaamini wanastahili kuwemo kwenye kikosi hicho: Mohamed Chuma, Jellah Mtagwa, Hamis Gaga, Willy Mwaijibe, Sunday Manara, Abdallah Kibadeni. Waweza kutaja kwa mfano kipa bora, centre half (namba 5) bora, namba tisa bora, n.k.
 
Back
Top Bottom