Taifa Stars vs Benin, 12 Oktoba 2014

Taifa Stars vs Benin, 12 Oktoba 2014

Katavi

Platinum Member
Joined
Aug 31, 2009
Posts
42,099
Reaction score
12,920
Walio mlio jirani na televisheni zenu na mna king'amuzi cha Azam mechi itaoneshwa laivu baada ya shamrashamra za mechi ya viongozi wa dini. Mechi itaanza saa 11 jioni.

Dk 16 Stars 1-0 Benin......canavaro.

Dk 40 stars 2-0 Benin....Kiemba.

Dk 50 stars 3-0...Ulimwengu.

Dk 70 stars 4-0.......Juma Luisio

Dk 89 stars 4-1 Benin.

FT Stars 4 - 1 Benin.

-----------------

MICHEZO TANZANIA 4-1 BENIN Timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars imeichapa timu ya Taifa ya Benin jumla ya mabao 4-1 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika Dimba la Taifa jijini DSM.

Wafungaji kwa upande wa Taifa Stars ni:- Nadir Haroub Canavaro kwa kichwa safi (16) Amri Kiemba kwa juhudi binafsi (40) Thomas Ulimwengu kwa kumalizia kros ya Mrisho Ngasa (49) Juma Luizio kwa kumalizia kazi kubwa ya Thomas Ulimwengu (71).
 
Timu zote mbili zipo uwanjani wakipasha misuli moto....
 
Mkuu tupe updates wengine hatuna azam

okay mkuu tuwe pamoja katika huu uzi.

Pinda anatoa hotuba kuwashukuru viongozi wa dini kwa mechi yao ya amani.
 
Naam mechi ya viongozi wa dini imeisha na sasa tunasubiri mechi ya stars na Benin,,,,,,,,,,LIVE katika Azam Two.
 
Uwanja umepwaya kweli kweli hakuna washabiki wengi.....
 
Hili bango la simba leo kwenye game ya taifa starz linakujaje!?
 
Timu ndio zinaingia uwanjani. Timu hizi zimekutana mara mbili na zote tumefungwa.
 
Nyimbo za taifa sasa zinapigwa hivi sasa wa Benin na wapo katika jezi nyeupe....
 
Mechi nyingine za Africa ni normal kuziona online, lakini hii haiwezekani, sijui kwanini!
 
Wimbo wa tanzania sasa na jezi zetu mpya...
 
Cannavaro ndio kapteni leo.
 
Match za TZ huwezi kuziona livescore.Tatizo ni nini?
 
Back
Top Bottom