Taifa stars coach | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taifa stars coach

Discussion in 'Sports' started by Mhamerd, Mar 26, 2011.

 1. M

  Mhamerd Member

  #1
  Mar 26, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu nina Mashaka na huyu kocha wa Taifa stars , Je tatafuzu kombe la Mataifa ya Afrika kwa Mtindo huu?. Tumesawazisha na sasa ni goli moja kwa moja lakini------.
   
 2. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  kwa hiyo unataka tukuulize swali "lakini nini?"
   
 3. only83

  only83 JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Acha umbea wewe..........mwacheni Mwalimu afanye kazi,soka letu linahitaji uvumilivu sana.Unajua soka la Ulaya kwasababu ya uwezo wachezaji waliojengewa ni rahisi kumlaumu Kocha timu inapoboronga.Hapa kwetu wachezaji wakiwa kwenye vilabu vyao ni upupu mtupu,huko ni majungu na vurugu,anapokuja timu ya Taifa mwalimu anaanza moja,tangu nidhamu,vyakula nk.Sasa hapo unategemea ushindi wa haraka kweli?
   
 4. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,056
  Likes Received: 299
  Trophy Points: 180
  Bado hatuna chama cha mpira chenye dira ya kweli hapa kwetu TZ. Bado hatuna vilabu vyenye kutoa mchango muafakaktk timu yetu ya Taifa. Bado shule yenye hadhi na malengo ya soka kitaifa. Bado wachezaji wetu wanavipaji vya soka bila elimu ya soka tangu wakiwa wadogo. Bado wachezaji wetu wamelala usingizi ktk kitanda cha makuzi ovyo ya kisoka na kulewa sifa mapema kabla ya mafanikio. Kwa mtaji huu hatwendi kokote katu. Mwalimu anakuta michezaji imekomaa 'ugoko' kiasi hawezi kuwanyoosha labda avunje kabsaaa!
   
 5. m

  matunge JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Tatizo la Tanzania si kocha. Ni wachezaji, wanaotokana na mfumo mbovu wa malezi ya kisoka tangu wakiwa watoto.Hii inafanya wasiwe na nidhamu ya soka,kujitambua na mambo mengi ya namna hiyo.Kwa hapa bongo hata akija Mourinho,Ferguson, ama Wenger mambo yatakuwa kama yalivyo_Ombi langu kwa serikali kupitia wizara husika.Ijaribu kutoa scholarship ya soka kwa watoto (chini ya miaka 17) wanaotokana na mashindano ya cocacola kila mwaka, wakasome katika academy za soka ulaya.Naamini tutafikia mafanikio tunayoyataka.Na hili linawezekana, utaratibu huu ukiendelea kwa michezo yote, TZ tutashinda katika michezo yote ikiwa ni pamoja na ile ya Olympic.Scholarships hizi ziwafikie pia makocha vijana na wachezaji wa zamani kama akina Chambua,Pawasa,Edibily baadaye waje wachukue mikoba ya kufundisha timu za Taifa.
   
Loading...