Taifa linahitaji Toba Kubwa

MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2016
Posts
15,741
Reaction score
39,784
Turudishe nyumba zote za msajili (NHC) tulizodhulumu (tulizotaifisha) kutoka kwa wageni na watu wetu . Turudishe mabenki, mashamba, viwanda, shule na taasisi zote tulizo dhulumu (taifisha) kutoka kwa wageni na wananchi wetu. Tuwaombe radhi na kuwalipa fidia watu wote waliodhulumiwa na mali zao kuharibiwa wakati wa Azimio la Arusha na operation vijiji.

Tufanye sala kuu ya toba, taifa limrudie Mungu, bila hivyo maendeleo tutayasikia redioni na kwenye television. Kwani, tulidhulumu watu na vilio vya watu hao waliodhulumiwa vinalitesa taifa letu. Taifa letu limebarikiwa na kila lililo jema lakini bahati mbaya, kwa sababu ya dhuluma hiyo, hakuna kinachotokea.

Muheshimiwa Raisi, hatujalogwa, ila tulidhulumu, sasa laana ya dhuluma hiyo ndiyo inayotutafuna. Turudishe mali zisizo zetu ili tuweze kufungua milango ya bahati kwa manufaa ya taifa letu.

Nawasilisha kwaajili ya mapovu baridi na moto.
 
Mimi huwa sielewe watu wanapozungumzia masuala ya laana au hoja zinazomtegemea au zinazobebwa na neno Mungu.

Mungu gani wanam'zungumzia..? huyu ambaye alikuwa akitazama waafrica wakitawaliwa kikatili na kuuliwa,kukatwa vichwa na wakoloni na Mambo ya kishenzi mengi waliofanyiwa watu weusi.

Jambo la muhimu ni kuwajibika, watu tuwajibike,watu wachukuliwe hatua,watu wasimame wapinge ushenzi na unyonyaji.


Yangu ni hayo mwenye macho na atazame na kutafakari.
 
Mwenye enzi Mungu alikwishasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa, ukisha lielewa hilo basi utachagua lililo sahihi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…