Taifa linaendeshwa na news | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taifa linaendeshwa na news

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Livanga, Jul 20, 2011.

 1. Livanga

  Livanga JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 15, 2010
  Messages: 458
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Ndugu zangu watanzania wenzangu hali ilivyo hapa ndani sio ilivyo nchi za pembezoni na hata europe ambako wawekezaji wengi wameonyesha waziwazi kukata tamaa ya kuja kuwekeza na hata ambao weshawekeza wanawaza kuondoka. Sasa wengi wanasema na ndio ilivyo hata kwa baadhi yetu hapa kwamba NCHI HII INAENDESHWA NA NEWS na hakuna cha kubisha hapa na kama watanzania tukiendelea na hali hii tutakuwa na hali mbaya zaidi kadiri siku zinavyozidi kwenda.

  Jaribu kujiuliza tu maswala kama ya richmond , meremeta ambayo Dr. Slaa alisimamia kidete sana alipokuwa mbunge, nyumba za serikali zilizouzwa kwa viongozi, mafao ya wazee wa EA, reli, ATC, vijisenti, kamati zilizoundwa kutokana na kashfa mbalimbali alizowahi kuzirise Dr. Slaa alipokuwa mbunge kesi za kina basil pesa mbili mramba na wenzake na mengine mengi ambayo nikiandika hapa uwezi kujibu yameishaje ila pale yanapotokea yanahit sana then wananchi tunapotezewa kiaina na tunasahau. hata hili la katibu wa MEM litapotea kimya bila hatua zozote kuchukuliwa na 1 bilioni tayari imeshaondoka .

  Tanzania tunakwenda wapi kama hali ndio hii je Wanaotuita taifa la news wanakosea na je tutegemee maendeleo yoyote kama hali ndio hii.

  kama unampenda swahiba yako usimpe ajira ya kuripoti kwako
   
 2. BASHADA

  BASHADA JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 487
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Sasa nani mjinga!! Acha kulaumu serikali, tujilaumu sisi wasahaulifu na mabumbumbu. Watanzania ni waoga and let them die natural death kama kondoo anayenyeshewa
   
 3. Livanga

  Livanga JF-Expert Member

  #3
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 15, 2010
  Messages: 458
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Sawa ni watanzania lakini sio wote wengine tunaongea sana ila wanatuunga mkono ni wachache ila one day tutaforce mtuunge mkono.
   
Loading...