Nanyaro Ephata
JF-Expert Member
- Jan 22, 2011
- 1,237
- 1,828
Taifa lipo njia panda likiweweseka,na hatari kuu za maangamizi.Nchi imekosa dira na mwelekeo wa maendeleo,uchumi wan chi
umelala.Tunaimbishwa wimbo wa ujamaa huku tukichezeshwa ngoma ya Ubebari.Taifa linakabiliwa na umomonyokaji mkubwa wa maadili na utamaduni,nchi inabugia makapi na sumu ya kila aina kwa maangamizi yake yenyewe.Taifa bila utamaduni na maadili yake ni sawa na mti bila mizizi.
Heshima ya mtanzania ndani nan je ya nchi imetoweka,udini umeshika kasi,na hata kutishia kuigawa nchi katika vipande vipande
Watanzania tumepokwa haki na uhuru wetu wa kitaifa,kwa maana ya kujitawala na hatma yetu bila kuingiliwa na watu wasio
wazalendo,tumepoteza uhuru dhidi ya magonjwa,uhuru dhidi ya njaa,uhuru wa kiuchumi.Kupotea kwa uhuru huu ni matokeo ya uchumi na rasilimali za nchi kumilikiwa na kikundi cha watu wachache,huku serikali dhaifu ikisalimu amri kwa genge hili la wahujumu wachache.
Watanzania wamepoteza uhuru binafsi,haki ya kuishi maisha ya heshima,haki ya kupata habari,usawa kwa wote.Eee Mtanzania amka kuwa sehemu ya mabaliko utakayo.
"Kuna nyakati unaweza kuchoka kupinga dhulma na uonevu katika jamii,lakini kamwe isitokee nyakati ukaacha kupinga dhulma na uonevu katika jamii"