SoC02 Taifa lianzishe kituo cha kuwakusanya wahitimu wa vyuo vikuu ambao ni wabunifu wa mifumo ya teknolojia

Stories of Change - 2022 Competition

Eng. Zezudu

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
7,817
10,858
UTANGULIZI

Katika Dunia ya sasa tekinolojia na ubunifu vimekuwa vyanzo vya maendeleo katika nchi mbalimbali, Leo hii Marekani, China, Urusi, India na nchi mbalimbali Duniani zimepiga hatua kimaendeleo sababu ya kuwekeza katika tekinolojia na ubunifu. Tekinolojia hizi zinazobuniwa huwekezwa kwa vijana na kurithishwa kwa vizazi vijavyo kupitia shughuli mbalimbali katika nchi husika.

Serikali imewekeza pesa nyingi kwa wahitimu wa elimu ya juu lakini kwa sasa Tanzania hatuna kituo ambacho kinawakusanya vijana mbalimbali hasa wanaohitimu vyuo vikuu walio na miradi mbalimbali ya kitekinolojia na ubunifu ili kuwawezesha kifedha na kuwasidia pale wanapo kwama Ili waweze kutimiza malengo yao. Ndoto izo hufa baada ya kumaliza chuo na kuanza kutafuta kazi Ili waweze kuishi.

Kwa sasa Tanzania inabodi mbalimbali zinazojihusisha na masuala ya kihandisi, bodi hizo asilimia kubwa zinahusika kukusanya ada na kusajili wahandisi, wakandarasi na wabunifu wa majengo. Lakini hatuna mkakati wa kudumu wa kutumia vipawa vyao vya ndani vya hao wahandisi zaidi ya kuwatafutia sehemu ya kupata ujuzi wa kazi na kukusanya ada.

Ubunifu utamjenga kijana kuacha kutegemea ajira kama ilivyo sasa ili awe mtu wa kuwaza kutengeneza ajira kwa wengine.

SABABU ZA KUANZISHA KITUO HICHI
Kutokana mfumo wa elimu wa nchi yetu. Asilimia kubwa ya mambo tunayofundishwa darasani hasa elimu ya uhandisi ni kuhusu jinsi gani kitu fulani kimetengenezwa, vitu na mahesabu yaliyotumika kutengeneza vitu ivyo ambayo asilimia kubwa mambo hayo yapo katika Dunia ya kwanza (nchi zilizoendelea) lakini hapa Tanzania tunachofundishwa darasani na tunachoenda kukifanyia kazi ni vitu viwili tofauti kitu ambacho kinasababisha wahitimu wengi kuoneka vilaza katika kazi na kwenye karatasi wako safi.

Pia ubunifu huanzia katika karatasi mpaka kitu halisi. Mfano ukiwa darasani Unaweza fundishwa jinsi ya kubuni na kutengeneza ugavi wa nguvu (power supply in English) lakini sehemu ya kazi utafundishwa jinsi ya kutumia iyo power supply. Hii inasababisha kichwa kuacha kufikiria zaidi ubunifuni ila kuhakikisha kazi za watu zinaenda na jinsi ya kuwasimamia wafanyakazi. Kutokana huo mfumo taifa linaendelea kutegemea tekinolojia mpya na ubunifu kutoka nchi za nje.

UMUHIMU WA TEKINOLOJIA NA UBUNIFU

1. Kilimo cha kisasa
Maendeleo ya tekinolojia na ubunifu wa kisasa unaweza kuwa chachu ya kuendeleza kilimo cha kisasa na kukuza uchumi na pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, hasa ukiwekeza katika umwagiliaji, matumizi ya zana na kisasa za kilimo na kubadilisha ardhi isiyo na rutuba na iliyojaa mawe au mchanga na kuwa na rutuba kwa kuweka udongo katika eneo husika ambao utaweza kustawisha mazao mbalimbali na mboga mboga.

Pia mtu anaweza kubuni hata mbinu ya kisasa ya kumwagilia maji shamba bila kufika eneo la shamba kwa kuandika misimbo ambayo itafunga na kufungua bomba za umwagiliaji maji shambani kwa kuangalia mda au unyevu katika ardhi.

2. Viwanda
Tekinolojia na ubunifu zinachangia kuendeleza viwanda na kuwa vya kisasa zaidi ambavyo vitatumia tekinolojia ya hali ya juu na kisasa hasa katika kuendesha viwanda Kwa kutumia mfumo ya kielectroniki mfano mtu anaweza kubuni mfumo utakao msaidia msaga mashine kujua kuwa kiasi cha umeme kinachopita katika mizunguko ya waya za Mota ni sawa au unaweza unguuza mota kwa kuweka msimbo kwamba machine ijizime yenyewe umeme ukiwa mdogo.

3. Ajira

Tekinolojia na ubunifu zitatengeneza ajira kwa watu walio buni mfumo wa tekinolojia husika.

JINA LA KITUO HICHI
Kitua hicho ambacho kitahusika kukusanya tekinolojia na ubunifu kiitwe jina hili
Technology and innovation collection centre ( TICC ).

Technology and innovation collection centre (TICC) ni kituo ambacho kitatumika kukusanya vijana mbalimbali ambao ni graduate wa fani mbalimbali za sayansi nchini na wanamawazo na ubunifu wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo au kuimarisha miradi iliyopo ili iwe ya kisasa zaidi.

MADHUMUNI YA KITUO CHA TECHNOLOGY AND INNOVATION COLLECTION CENTRE (TICC)

Kuwawezesha vijana kifedha na kimawazo katika kuboresha ubunifu wao kwa kukutana na wataalamu mbalimbali ambao ni wazoefu katika kufanya ubunifu.Kusaidiana na wataalamu mbalimbali ili kutatua changomoto zinazojitokeza katika miradi yao waliobuni. Kwa sasa vijana wengi ubunifu wao unaishia mashuleni na vyuoni hakuna mkakati madhubuti wa serikali kuwaendeleza vijana ambao wanatoka vyuoni na hata ambao wako mtaani pia.

Mana wahitimu wa vyuo walifanya miradi ya ubunifu vyuoni, miradi hiyo huishia huko huko vyuoni na inabaki mali ya chuo, lakini mara nyingi ubunifu unakuwa hauja ishia hapo chuoni . Ubunifu ni endelevu kwa vijana hata wakiwa mtaani ,lakini kutokana na familia nyingi za kitanzania ni maskini zinashindwa kuwaendeleza vijana wao katika masuala ya ubunifu.

Kuleta ushindani na kiu miongoni mwa wahitimu kubuni mifumo ya kisasa zaidi na imara, pindi kundi la wabunifu litakapo kuwa pamoja lazima kila mtu atapambana kuleta kitu cha kisasa na bora zaidi ya mwenzake.

Kuwaandalia mazingira ya kufanyia kazi ( maabara na karakana ). Karakana na maabara ni muhimu katika kuendeleza sayansi na tekinolojia, hasa Kwa ujenzi wa kitu halisi kilichobuniwa na kuonesha ni jinsi gani kinafanya kazi.

Kuwapatia vifaa na program za compyuta ambazo zitawasaidia katika ubunifu.
Vifaa na program za kisayansi ni gharama sana ambapo kwa mtu wa kawaida anashindwa kumudu kuwa navyo kwa ajili ya kufanyia shughuli zake za ubunifu.

Kuandaa vijana ambao wataenda kufanya kazi nchi ziilizo endeleaje kwa dhumuni la kupata ujuzi na ufahamu kutoka huko ili kuja kuwatumia nchini na kuwa fundisha vijana waliopo nchini kwa vitendo. Kumbuka nchi mbalimbali zinatumia majasusi kuenda kuiba tekinolojia.

Kuingia ubia na mataifa makubwa hasa yaliyoendelea katika tekinolojia ili yaweze kuleta wataalamu wao hapa nchini na tuweze kuwatumia katika shughuli za ubunifu.

MFUMO WA UENDESHAJI WA TECHNOLOGY AND INNOVATION COLLECTION CENTRE

Chanzo cha mapato

Kituo hichi kinaweza kuendeshwa kwa serikali kutenga bajeti ya kutosha ili kuwezesha ufanikishaji, upatikanaji wa vifaa ambayo vitatumika katika tekinolojia na ubunifu.

Fedha za tozo kupelekwa katika kituo hichi kwa sababu tunahitaji kutengeneza taifa linalo jitegemea, Mana ukitegemea pesa kutoka nje , wazungu watakuwa washazipangia zitumike wapi na kuwapa mipaka kibao ya matumizi . Taifa litumie fedha za tozo kama mtaji katika kufanikisha hili.

Unapokuwa na tekinolojia na kuiuza lazima utatengeneza mapato ya kuendesha shughuli husika na kurudisha pesa ulizowekeza katika tekinolojia na ubunifu husika na mwisho wa siku kuondoka na utegemezi wa nje.

Utawala

Ili shughuli yoyote iendelee inahitaji uongozi imara , uongozi imara ni chachu ya maendeleo katika sekta yoyote Ile ya kijamii.

Faida za technology and innovation collection centre

Kufufua viwanda vilivyo kufa
Baada ya kuondoka wakoloni nchi Yetu iliachiwa viwanda vingi ambapo mpaka Sasa vingi havifanyi kazi, kupitia hichi kituo tutakuwa na wataalamu ambao wata study mfumo wa ufanyaji kazi wa ivi viwanda vilivyo kufa na kuvifufua au kuangalia namna ya kuboresha mifumo hii ili iwe ya kisasa zaidi.

Kuzalisha wataalamu wa kutosha ambao watatumika katika kuboresha mifumo mbali Mbali ya kiulinzi, viwanda ,kilimo Cha umwagiliaji.

Hitimisho
Kutokana na sera ya taifa kuwa halifungamani na upande wowote; leo hii kama taifa lingekuwa linajitegemea tusingepangiwa nchi rafiki, nchi ipi adui, wapi tununue mafuta wapi tusinunue na maamuzi ya taifa yangeheshimika.

Tujitegemee kuepuka utumwa na ukoloni maomboleo vinginevyo tuendelee kuwa tegemezi na watumwa huru wenye uhuru wa bendera na demokrasia ya kizushi. Kupanga ni kuchagua naomba mpigie kura bandiko hili na tufute utegemezi nchini.
 
Costech si Wana hub Kwa ajili ya wabunifu inaitwa bunihub?
https://costech.or.tz/read/submenu/innovation-spaces

Nadhani unachokizungumzia wewe ni uwekezaji zaidi kwenye R&D ambayo inahitaji pesa nyingi lakini pia hatua za mwanzoni teknolojia huwa inasafirishwa au kuibiwa toka nchi zingine kama walivyofanyaga USA na sasa China.

Sidhani kama TZ Kwa sasa ina msuri WA kuunda cutting edge technology yenyewe bila kufanya juhudi ya ku-import toka nje kitu ambacho hakifanyiki.
 
Wazo zuri pia serikali ianzishe app center ya kukusanya maoni ya kuendeshea nchi,na kutatua changamoto mbalimbali za nchi.Nchi haiwezi kwenda kwa kutegemea mawazo ya viongozi wachache ambao wakipata nafasi uwezo wa kufikiri unapungua sababu ya kupewa kila kitu bure kupitia kodi zetu. Watu walio nje ya mfumo wa maamuzi Wana mawazo mengi Sana mazuri yawezayo leta mabadiliko nchini lakini watayatolea wapi?
Mfano mimi ninao mchanganuo wa
1.Kuzalisha nishati na mafuta mbadala Ili tuache kuagiza mafuta na nishati nje ya nchi Ili pesa zibakie nchini zifanye uzalishaji kuliko kuzitupa nje.
2.Kuondoa na kumaliza tatizo la ajira nchini.
3.Ujenzi wa nyumbani bora kwa gharama nafuu na kufuta nyumba za udongo Ili KILA mtza apate nyumba bora.
4.Mpango bora wa matumizi ya ardhi.
5.Mpango wezeshi kwa vijana waone fursa tele zilizojaa nchini na sio zinaonwa na wageni tu.
6.Vyanzo mbadala vya kupata pesa za kuendesha nchi pasipo kulazimika kuwakamua wananchi kupitia kodi na tozo au mikopo.
7..Na zingine nyingi.
Watz wengi tu wanayo mawazo mazuri kabisa ambayo yakitumika vyema yataleta positive changes kwenye Jamii.
 
Ni kweli tekinolojia inaibiwa , ndo Mana hapo juu nimesema Tanzania iandae hata vijana ambao wataenda kufanya ujasusi wa tekinolojia katika nchi za ughaibuni.
 
Kuhitimu ni nini bwana. Ubunifu ndio kila kitu.
 
Tz hapana isee serikali yetu ipo radhi ikusanye vijana wote wa ccm na kuwalisha ila sio hayo mambo ya tech sijui nini..

Wewe pamban kivyako tu ukitoboa ndio viongozi watakuchekechekea na kujifanya wanakujua sana.

Ila sometimes mambo yanayofanywa nchini hapa yanaumiza mnooo.
 
Wazo zuri pia serikali ianzishe app center ya kukusanya maoni ya kuendeshea nchi,na kutatua changamoto mbalimbali za nchi.Nchi haiwezi kwenda kwa kutegemea mawazo ya viongozi wachache ambao wakipata nafasi uwezo wa kufikiri unapungua sababu ya kupewa kila kitu bure kupitia kodi zetu. Watu walio nje ya mfumo wa maamuzi Wana mawazo mengi Sana mazuri yawezayo leta mabadiliko nchini lakini watayatolea wapi?
Mfano mimi ninao mchanganuo wa
1.Kuzalisha nishati na mafuta mbadala Ili tuache kuagiza mafuta na nishati nje ya nchi Ili pesa zibakie nchini zifanye uzalishaji kuliko kuzitupa nje.
2.Kuondoa na kumaliza tatizo la ajira nchini.
3.Ujenzi wa nyumbani bora kwa gharama nafuu na kufuta nyumba za udongo Ili KILA mtza apate nyumba bora.
4.Mpango bora wa matumizi ya ardhi.
5.Mpango wezeshi kwa vijana waone fursa tele zilizojaa nchini na sio zinaonwa na wageni tu.
6.Vyanzo mbadala vya kupata pesa za kuendesha nchi pasipo kulazimika kuwakamua wananchi kupitia kodi na tozo au mikopo.
7..Na zingine nyingi.
Watz wengi tu wanayo mawazo mazuri kabisa ambayo yakitumika vyema yataleta positive changes kwenye Jamii.
Kweli kabisa nazani kikwazo kikubwa ni mtaji na upatikanaji wa huo mtaji, ndo mana tunahitaji serikali iwe inatoa pesa kwa ajili ya kuwasaidia wabunifu kutimiza malengo yao.
 
Wazo zuri Sana yani Sana lakini kwa hawa walamba asali ni kama kumpigia mbuzi gitaa ukitegemea atacheza, wao wanawaza zaidi kunenepesha vitabu vyao vya benki
 
Wale bachelor of arts je?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata hawa nao huwa wanafikiria mawazo ya kiubunifu lakini hawafahamu ni jinsi gani wanaweza kulifanyia implementation, wakipeleka ili wazo katika kituo hichi litafanyiwa kazi. Na mleta wazo anapewa feedback kwamba wazo lake linawezekana au haliwezekani.
 
Kweli kabisa nazani kikwazo kikubwa ni mtaji na upatikanaji wa huo mtaji, ndo mana tunahitaji serikali iwe inatoa pesa kwa ajili ya kuwasaidia wabunifu kutimiza malengo yao.
True wabunifu wapo wengi sana wangeweza leta positive changes kwenye Jamii.Mfano pana mtu kagundua formula ya kuzalisha cement yenye ubora zaidi tena kwa gharama nafuu zaidi,mfuko kg 50 anauza kwa elf 7.
 
Tz hapana isee serikali yetu ipo radhi ikusanye vijana wote wa ccm na kuwalisha ila sio hayo mambo ya tech sijui nini..

Wewe pamban kivyako tu ukitoboa ndio viongozi watakuchekechekea na kujifanya wanakujua sana.

Ila sometimes mambo yanayofanywa nchini hapa yanaumiza mnooo.
Kweli kabisa hata zile 7500 wanazopewa vijana wa kusifu na kuabudu , zingetumika katika mambo ya ubunifu na kuwawezesha vijana
 
True wabunifu wapo wengi sana wangeweza leta positive changes kwenye Jamii.Mfano pana mtu kagundua formula ya kuzalisha cement yenye ubora zaidi tena kwa gharama nafuu zaidi,mfuko kg 50 anauza kwa elf 7.
Safi kabisa watu kama Hawa ilitakiwa wawe wanaangaliwa kwa jicho la tatu Ili waweze kusaidiwa mitaji na waongeze uzalishaji wa hizo cement, shida ni kuwa walamba asali katika ivyo viwanda wanakwamisha , unashangaa wanamkamta kwamba halipi Kodi.
 
Mchina anajenga kiwanda kikubwa cha cement tanga uenda bei ikashuka
 
Bei kushuka ni kazi mana wazee wa viwanda wanakutana kupanga bei, ili bei zisitofautiane sana, kama wanavyofanya mitandao ya simu
 
Kwa wachina labda wapigwe biti,Wachina ni waumini wa uza bei ndogo uuze kwa wingi mara nyingi Ili upate faida, pia sio waumini wa mzigo kujazana godown
 
Back
Top Bottom