MIXOLOGIST
JF-Expert Member
- Mar 1, 2016
- 12,695
- 31,475
Habari za asubuhi wana JF
Kwa masikitiko kabisa naomba niwasilishe hii hoja chungu. Taifa letu limejaa watu wanafki na wenye husda. Ni jambo la kawaida kabisa kuona watu wakimshangilia kiongozi au mtu mwenye pesa ambaye anafanya mambo ambayo siyo sahihi. Sehemu kubwa ya watu wetu ni watu waoga wenye tabia za kujipendekeza. Jamii yetu imejaa watu ambao furaha yao inakamilika pale ambapo mtu mwingine anaharibikiwa. Ikiwa mtu amefukuzwa kazi, au amefilisika, au amepatwa na matatizo basi jamii yetu inapata furaha.
Haya mambo ni ya hovyo kabisa kwenye jamii yoyote ile na kamwe taifa haliwezi kuendelea likiwa limesheheni watu wenye husda na unafki. Kwa mamtiki hiyo, itatuchukua miaka mingi sana kupata maendeleo tukiwa tunaendekeza wanafki na watu wenye husda. Watu wa aina hii wanarudisha maendeleo yetu nyuma. Kuna baadhi ya nchi kwenye bara la ulaya haswa karne zilizopita waliamua kuwaua wanafki, wachamwi (watu wenye husda) na washirikina wote. Hivyo basi, ni lazima tuwatambue wanafki na watu wenye husda kama ni maadau wa taifa letu na ndiyo watu wanaoturudisha nyuma kimaendeleo. NAOMBA KUWASILISHA, mapovu yanaruhusiwa.