Taifa la wachakachuaji,je tunaaminika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Taifa la wachakachuaji,je tunaaminika?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andrew Kellei, May 27, 2011.

 1. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #1
  May 27, 2011
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Salaam wakuu,
  Katika kupitia magazeti ya wiki,nilikutana na makala ya MSOMAJI RAIA kwenye gazeti la Raia Mwema yenye kichwa cha habari SAKATA LA CHENJI YA RADA,naomba tuitazame kwa jicho la tofauti sehemu hii,
  "Kwanini kila kitu chetu hivi sasa ndani na nje kinatiliwa shaka kwa sababu ya uwezekano wa kuchakachuliwa? Mafuta yanachakachuliwa,kura zinachakachuliwa,mitihani inachakachuliwa,vibali vya kuzika maiti na vyeti vya kuzaliwa vinachakachuliwa,ghala za silaha zinachakachuliwa,operesheni za vichwa muhimbili zinachakachuliwa,tafiti zinachakachuliwa,hukumu zinachakachuliwa,naam hata ziara za raisi zinachakachuliwa! Huu uchakakachuaji hauwezi kulifanya taifa liaminike mbele ya umma wa kimataifa,na hasa katika suala nyeti kama la chenji za ununuzi wa rada uliochakachuliwa"
  Sasa kama hali ndo hii,upo uwezekano mkubwa wa mambo mengi kuendelea kuchakachuliwa na kuaminika ndivyo kunavyozidi kupotea.
  Nini hatima ya yote haya,tufanye nini kurejesha imani?
   
 2. Andrew Kellei

  Andrew Kellei JF Gold Member

  #2
  May 28, 2011
  Joined: Sep 11, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mbona mmeichunia?
   
Loading...