chitalula
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 1,302
- 415
JUMUIYA ya Taasisi ya Elimu ya Juu Tanzania (Tahliso), imegomea mkakati wa kutumiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kutoa matamko ya kuvishambulia vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Tanzania Daima Jumatano limedokezwa kuwa baada ya mpango huo kukwama, makada wa CCM wamefadhili mgogoro ndani ya jumuiya hiyo ili kumngo Mwenyekiti wa sasa, Musa Mdede akidaiwa kuendesha uongozi kisiasa.
Hii si mara kwanza Tahliso kugoma kutumiwa na CCM. Mwaka jana, wakati rasimu ya kwanza ya katiba ikijadiliwa kwenye ngazi ya mabaraza, mmoja wa makada wa CCM anayetajwa kutaka kugombea urais 2015, alijaribu kujipenyeza bila mafanikio.
Kada huyo aliingilia mkutano wa baraza la katiba la Tahliso lililokutana mkoni Mbeya, akitaka kuwarubuni viongozi watoe tamko la kupendekeza kuunga mkono umri wa mgombea urais upunguzwe kutoka miaka 40 ya sasa hadi 35.
Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa Tahliso walishtukia uchafu huo na kumzuia kada huyo aliyekuwa amealikwa kinyemera kufunga kikao chao asiingie ukumbini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, kuhusu mkakati huo unaoendeshwa na kundi lingine, Mdede aliwataja viongozi wa CCM wanataka kuwavuruga kwa maslahi ya kundi lao la urais wa 2015.
Amtaja Katibu wa Chipukizi na Uhamasishaji wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Taifa, Paul Makonda na Katibu wa CCM mkoa wa Vyuo Vikuu, Chrstopher Ngubiagai.
Mdede alisema baada ya uongozi wake kuingia madarakani Desemba mwaka jana, amekuwa akipokea simu mbali mbali kutoka kwa viongozi waandamizi wa CCM wakimtaka kutoa kauli katika baadhi ya mambo jambo ambalo alilipinga.
Viongozi waandamizi wa CCM wamekuwa wakinipigia simu kila mara nitoe matamko ya kisiasa. Mimi jibu langu kwao lilikuwa ni moja tu kuwa taasisi yetu si sabuni ya kuwasafishia watu wanaoutaka urais,
Niliwaambia kuwa Tahliso si kisemeo cha chama chochote cha siasa bali ni taasisi iliyopo kwa ajili ya maslahi ya wanafunzi wa elimu ya juu,alisema.
Mdede alifafanua kuwa hata taarifa zilizotolewa hivi karibuni kuwa uongozi wao umeondolewa madarakani si sahihi kwa sababu mkutano uliofanyika Chuo cha Kodi jijini hapa haukumalizika kutokana na fujo zilizojitokeza.
Aliongeza kuwa baada ya kuahirishwa kwa mkutano huo kikundi cha watu kilijikusanya sehemu na kutoa tamko kama wanachuo.
Alisisitiza kuwa CCM imekuwa na utamaduni wa kuitumia Tahliso kukamilisha azma mbali mbali za kisiasa na kwamba baada ya uongozi wake kuingia madarakani jambo hilo alilipiga marufuku hali iliyomtengenezea uaduni na wenzake.
Katika kuhakikisha tunaondolewa madarakani, vikao kadhaa vilifanyika vikiongozwa na Ngubiagai. Kikao cha kwanza kilifanyika Januari 28 mwaka huu katika hoteli ya (anaitaja) iliyopo Magomeni na kingine kufanyika (anataja),alisema.
Aliongeza kuwa ushawishi alioambiwa aufanye kwa vijana wanaotarajia kuhitimu hivi karibuni ni kwamba wajiunge na CCM kwa ajili ya kupatiwa ajira.
Chanzo: Tanzania daima
MAONI YANGU:
Walau sasa TAHLISO imepata watu wenye msimamo, hii itawajengea heshima sana kwa wananchi, ni jambo la aibu sana wasomi wetu kutumiwa na wanasiasa uchwara, tukumbuke pia tahliso iliyumba sn kwa kutumiwa na ccm mpaka baadhi ya vyuo vilijitoa na kuanzisha umoja mwingine.
Tunawapongeza sana muendelee na msimamo huohuo