TAHLISO: Taarifa kwa wanafunzi wa elimu ya juu

TAHLISO: Taarifa kwa wanafunzi wa elimu ya juu

RGforever

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2011
Posts
6,877
Reaction score
5,446
JUMUIA YA WANAFUNZI WA TAASISI ZA ELIMU YA JUU TANZANIA (TAHLISO)

TAARIFA KWA WANAFUNZI WA TAASISI ZA ELIMU YA JUU

YAH: MUONGOZO WA UTOAJI MIKOPO ULIOTOLEWA NA WIZARA YA ELIMU , SAYANSI NA TEKINOLOJIA.

Jumuia ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya juu Tanzania (TAHLISO) inawataarifu wanafunzi wote wa vyuo vikuu namna ilivyoshughulikia na kupata utatuzi wa Muongozo uliotolewa na Wizara kama ifuatavyo.
Waraka uliotolewa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Tarehe 14/10/2016 ulitoa ufafanuzi namna mkopo utakavyotolewa kwa mwaka huu 2016/2017 kwa wanafunzi wapya wanaojiunga na masomo kwa mwaka huu “kuanzia mwaka huu wa masomo ,wanufaikawote wa mikopo (wapya na wanaoendelea na masomo)watakopeshwa kulingana na uwezo wao (means tested) katika vipengele vyote vya mkopo” Kufuatia maelezo hayo ni dhahiri mikopo kwa wanafunzi wanaoendele hasa kwa wale wenye wazazi bila kujali anauwezo ama hana uwezo mikopo yao ingepungua kutoka kwenye asilimia walizopangiwa awali, hata hivyo kwa muongozo huo ungepelekea fedha inayotolewa kwa ajili ya chakula na malazi (boom) kupungua jambo ambalo lingepelekea wanafunzi wengi kushindwa kuendelea na masomo kutokana na uwezo wa familia wanazotoka hasa watoto wa maskini ambao hutegemea fedha hizohizo za boom kulipia sehemu ya ada iliyobakia na huku wakiendelea kuishi maisha ya shida vyuoni.
TAHLISO ambayo ndio chombo cha kutetea maslahi ya wanafunzi wote wa vyuo vikuu tumeliingilia kati swala hilo kwa kufanya mazungumzo na uongozi wa bodi ya mikopo HESLB pamoja na mh.Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Ndalichako juu ya kubadili msimamo wa muongozo huo kwakua utawaathiri wanafunzi wengi ambao ni watoto wa maskini.
Katika majadiliano yetu yaliongozwa na hoja mbili zinazohusu wadahiliwa wapya na wanaoendelea na masomo, tumekubalina yafuatayo:

1. Muongozo mpya wa utoaji mikopo uliotolewa kwa mwaka huu wa masomo 206/2017 utawahusu wadahiliwa wapya wanaoanza masomo.

2. Wanafunzi wanaonufaika na mikopo wanaoendelea na masomo wao wataendelea na utaratibu kama ulivyokuwa tangu awali walivyoingia makubaliano na utaratibu mpya hautawaathiri.
Hata hivyo zoezi la serikali la kuhakikisha kwamba kila mwanafunzi mnufaika anayestahili kupata mkopo anapata mkopo wake.
Aidha kufuatia Tangazo la Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia lililotolewa tarehe 17/10/2016 linalohusu uhakiki wa wanafunzi wanaoendela na masomo ya shahada zoezi litakalofanyika kwa wiki mbili kuanzia tarehe 19/10/2016. TAHLISO inaomba kila mwanafunzi anayesoma shahada kuangalia majina yaliyotolewa kwenye tovuti ya TCU ili kuhakikisha jina lake lipo,na kwa yule ambaye hataona jina lake awasiliane na uongozi wa TCU haraka iwezekanavyo ndani ya wiki hizo mbili kuanzia tarehe tajwa hapo juu ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza.



STANSLAUS PETER KADUGALIZE
MWENYEKITI WA TAHLISO
 
Aiseeeee, Tahliso!! Hiyo ndio taarifa kwa Umma!! Kweli mwenyekiti mnae na sijui mlimchagua vipi? Huyu amebaliki continuing students warudishe makwao how sure kwamba uhakiki wa mwanzo ulikuwa unamapungufu?? How sure kwamba uhakiki wa sasa tena wa wiki mbili utakuwa sahihi?? Bora mie nilisoma enzi zile Nimrod akiwa bodi ya mikopo, yaani tukigoma kidogo jamaa anatukopesha zake, na kipindi hicho kulikuwa na unit ya kutosha,
 
Mimi nilidhani mtauchallenge muongozo mpya ubadilishwe kumbe mmewashushia zigo madogo wa festi yia.....So techmically, mlichoenda kusema ni kuwa nyie muachwe mmalize chuo ila hao wanaokuja ndo wapewe hadi boom na stationary kwa asilimia
 
Aiseeeee, Tahliso!! Hiyo ndio taarifa kwa Umma!! Kweli mwenyekiti mnae na sijui mlimchagua vipi? Huyu amebaliki continuing students warudishe makwao how sure kwamba uhakiki wa mwanzo ulikuwa unamapungufu?? How sure kwamba uhakiki wa sasa tena wa wiki mbili utakuwa sahihi?? Bora mie nilisoma enzi zile Nimrod akiwa bodi ya mikopo, yaani tukigoma kidogo jamaa anatukopesha zake, na kipindi hicho kulikuwa na unit ya kutosha,
Kama ulienda chuo kwa sifa stahiki wasi wasi wako nini..
 
"Jumuia" badala ya "Jumuiya"
Inadhihirisha wasomi wa siku hizi wavivu
 
Sioni umuhimu wa alichokiongea kwa kutetea wanafunzi waliopo chuoni na sio wanaoingia ko kwa maelezo kbsa inaonesha dhahiri hawako bega kwa bega na vijana wanaoingia chuoni sahivi kwa maelezo aliyoyasema hapo juu ,hii ndo dunia yetu ambayo watu wako bize kutetea maslahi yao wenyewe na sio ndugu zao
 
Enzi hizo DARUSO ndo kilikuwa chombo kinachotoa mwongozo kwenye vyuo vingine jinsi ya kudai haki zao.

Waliobaki ni kujikombakomba tu.
 
Sijawahi kuona mwenyekiti mpumbavu kama huyu
Ashindwe na anyong'onyee kwa jina la mizimu
 
Hajawasaidia wadogo zake hata kidogo bali kajiangalia yeye na wenzie wanaomaliza,kweli uongozi umevamiwa...
 
TAHILSO ya sasa haina tofauti na UVCCM ambao wao huwaza kupiga pesa tu
 
First Year huyo amepewa 77,000 yupo SUA...


152e8e0bd3f0a0f523953e3316c5d127.jpg
 
Stani kweli shida kabisa, yeye anaangalia tu maslahi yake, hili balaa vijana wetu hawa wakiwa viongozi ni shida kweli kweli.
 
Back
Top Bottom