Taharuki ya ujambazi kata ya Lulanzi-Kibaha, IGP na jeshi la polisi

magombe junior

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
2,016
1,036
Ni kata ya lulanzi maarufu kwa jina la chacha wilayan kibaha mkoa wa pwan wananchi wamejikuta wakiish maisha ya wasi wasi nakutokujua hatma yao baada ya majambazi kuweka kambi katika kata hiyo,ilianza siku wa jumamosi ya tarehe 7/2mida ya saa nane kasoro usiku tulisikia mlango ukivunjwa na watu kuanza kupiga kelele,ilikuwa ni nyumba ya jirani ambae ni dada anaejishugulisha za uuzaji vinywaji vya jumla alivamiwa na kundi kubwa la watu(wasiopungua 15) na kuamrishwa atoe pesa za mauzo

Kwa sababu ni karibu tulisikia majibizano kati ya majambazi na huyo dada,hatukuweza kujua kilichoendelea zaid kilichofuata tulianza kusikia milio ya risas uku majambaz wakiongea kwa saut kubwa kua mwenye uwezo atoke nje,ilikuwa ni kauli ya vitisho kwa sisi majirani ili tusitoke kutoa msaada,milio ya silaa iliendelea mpaka wakaondoka,baada ya kupambazuka tulisikia kuwa mama yake na yule dada alievamiwa usiku amejeruhiwa na wamempeleka hospitali

usiku wa jumatatu jana kuuamkia leo nyumbani kwetu mida ya saa sita usiku,kundi kubwa la mjambazi lilizingira madirishani na kuanza kuchungulia,baba aliwaona kupitia dirishani wanawasiliana kwa kupigiana simu na kupeana maelekezo walichungulia kila chumba ilikuwa kama wameshindwa kuingia na wakaonyesha kupanga kurudi na ni watu walewale inavyoonekana sababu walikuwa wengi kama wale wa mwanzo, hadi sasa familia yetu na zajirani tupo mashakani tusijue hatma yetu na maisha yetu.

Taarifa za uvamizi wa majambaz hawa zimefikishwa kituo cha polisi lakin chakushangaza hakuna hatua zozote za dharura zinazochukuliwa na jeshi il katika katika kuzua uhalifu huu usiendelee ,viongozi wa serikali ya mtaa nao hawaonyeshi ushirikiano ukitoa taarifa hawaonyeshi kushtushwa

Tunafaham kuna viongozi wakubwa wa nchi pamoja IGP ambao wanapata fursa yakuingia humu..tunaomba kulifikisha kwenu il walau kuanzia usiku wa leo tupate ulinzi na kulala kwa amani km watanzania wengine
 
Sasa wewe kama uliwaona na kuliko majibizano na huyo dada muuza vinywaji kwanini usipige simu polisi?
 
Back
Top Bottom