Tahariri kwachafuka tena wanataka kieleweke

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
[h=3]Chanzo: mpayukaji blog[/h]

_59767627_tahrircrowds.jpg

Umati wa watu kwenye viwanja vya Taharir mjini Cairo unaoandamana kushinikiza utawala wa kijeshi uachie ngaziuachie ngazi.
167109_175117322524527_135719259797667_317209_3652943_n.jpg

Wamisri wameamka tena na kurejea uwanja wa Taharir kudai serikali ya kijeshi ambayo wanaiona kama mwendelezo wa serikali ya Hosni Mubarak iondoke madarakani ili kukamilisha mapinduzi matakatifu ya umma. Inashangaza kuona wenzetu wanathubutu tena si mara moja wala mbili. Je watanzania tunaoteseka kuliko hata hao wamisri ambao wana maisha ya uhakika ikilinganishwa na yetu tulirogwa na nani? Je ni lini tutaamka na kufikiri kama watu na taifa kwa maslahi ya vizazi vijavyo? Je tumepata somo gani toka Misri? Wenzetu wana huduma kama umeme, maji,simu hata afya za uhakika kuliko sisi lakini bado wanaingia mitaani kutaka maisha bora zaidi. Sisi tumekuwa watu wa kupokea taarifa za maangamizi ambapo mabilioni shilingi yanavujwa au kuibiwa kila uchao nasi tunaangalia tu. Hatuna umeme wa uhakika pamoja na kuwa na vyanzo vingi vya umeme. Hatuna huduma za afya za maana. Makampuni ya nishati na mawasiliano yanatulangua na kutuibia kama vile hatuna akili wala macho. Wakubwa wanazidi kuchuuza na kugawana nchi yetu. Wanatanua wao na vizazi vyao wakati sisi tukiendelea kuteketea. Je ni lini tutaacha kuwa punda wa kubeba mizigo ya watawala? Inauma sana. Lazima tuanze kuhiari kujikomboa toka mikononi mwa genge la watu wachache. Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA.

polisi%2Bwakidhibiti%2Bwaandamanaji.jpg
 
Hawa wenzetu kiupeo wapo hatua kumi mbele yetu. Wanelewa nini maana ya utawala wa watu na wanataka wajitawale kwa kuzingatia utu wao na uwajibikaji wa viongozi wao
 
ukitaka ulie na roho yako tembelea tabora.
Nimesoma pale kamanda. Miaka nenda rudi Mkoa haubadiliki!!!!! Mabadiliko pekee yanayojitokeza ni ya kurudi nyuma zaidi, na cha kushangaza zaid,wananchi wamewapatia CCM majimbo yote ya Mkoa huu!!!! (Kati ya ngome za CCM na Mkoa wa Tabora unaongoza)

Yaan mtu yule yule aliyekunyima maendeleo kwa miaka 50 ya uhuru bado unataka akuongozee!!? Kweli silaha ya CCM ni ujinga wa wananchi
 
Tanzania hatuna rais. JK ni waziri wa mambo ya nje.
Kumbuka mkutano wa juzi brazil ulihudhuriwa na mawaziri wa mambo ya nje
CCM isha Jifia, nasikia Mkw'ere kisha hamia Obrigado Brazil, na harudi tena huku.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom