Tahariri: Chiligati assingize nchi katika Vita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tahariri: Chiligati assingize nchi katika Vita

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Mar 30, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,205
  Trophy Points: 280


  Tahariri:
  Mwanahalisi

  KATIBU Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Chiligati amejenga mazingira ya kutumbukiza taifa katika janga kubwa la vita.

  Aliwaambia waandishi wa habari mjini Dar es Salaam wiki iliyopita kwamba Watanzania hawataki kusikiliza taarifa za wizi wa fedha zao serikalini.

  Chiligati anasema wananchi wakizisikia taarifa hizo, hasa wanachama wa CCM aliodai wanazidi milioni nne, “watachukizwa” na hivyo kuamua kuchukua hatua za “kulipiza kisasi” kwa kuanzisha mapambano.

  Hoja ya Chiligati ni kwamba yeye na viongozi wenzake katika CCM, wanakerwa kusikia viongozi wa upinzani wakihusisha chama hicho na ufisadi uliotamalaki serikalini na nchini kote.

  Anataka wakome, vinginevyo watasababisha wanachama wa CCM kukasirika na matokeo yake watachukua hatua ya kulipiza kisasi.

  Kauli ya Chiligati inaashiria hatari. Ni kauli ya kuchochea wanachama wa chama chake. Kuwajaza pumzi, jeuri na kiburi ambavyo ni silaha za awali katika vita dhidi ya wananchi wenzao. Mauaji ya kimbari huanza hivyo.

  Chiligati ni mtu mkubwa serikalini; ni waziri anayekaa kwenye Baraza la Mawaziri. Vilevile ni kiongozi mkubwa katika chama anayeeneza sera, ilani na matakwa ya chama ambacho kimekuwa madarakani kwa zaidi ya robo karne.

  Uzoefu tulionao ni kwamba mara nyingi, kauli-amri za chama tawala zimechukuliwa kuwa maagizo ya kufanyia kazi. Ni kauli hizo ambazo zimewaelekeza wananchi na hata vyombo vya ulinzi na usalama: fanya hili, acha lile. Ni utamaduni uliojengeka.

  Leo hii, kwa kauli ya sasa ya Chiligati, hatuna sababu ya kutoamini kwamba anaandaa jeshi kubwa la wanachama milioni nne wa CCM, la kupambana na kila anayekosoa, anayekejeli, anayelaumu, anayelalamikia, anayetuhumu na hata anayeshitaki chama hicho kwa lolote lile.

  Hii ni hatari inayotokana na mchoko na kuishiwa uvumilivu wa kisiasa, wakati ambapo chama husika kingekuwa kinatumia shutuma na tuhuma kujisafisha na kujiandaa kwa ushindani na kwenye uwanja linganifu usio na vitisho.

  Ubabe huu, siyo tu utazaa vita alivyotangaza Chiligati, bali pia utaendelea kuthibitisha hulka ya chama hicho ya kutaka kushinda “kwa vyovyote vile.”

  Mara hii Chiligati anaahidi utawala wa kibabe utokanao na vita. Tunaukataa!
   
 2. n

  nzala Member

  #2
  Mar 30, 2009
  Joined: Dec 24, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mkuu hiyo mwanahalisi ya lini?ya kesho au last week?
   
 3. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Kumbe CCM ina wanachama ambao hawafiki hata 5 Mill! (30% ya wapiga kura)! Sasa sijui inakuwaje kwenye chaguzi wanapata 90% ya viti vya ubunge??????????????????
   
 4. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Wengi tu wanasubiri Nchi ichafuke maana nikisikia vuguvugu limeanza basi nitakuwa sichezi mbali na yale maduka yanayouza basikeli na mapikipiki bila ya kusahau yale ya majenereta ,ni wizi tu ,sa ikiwa viongozi ni wezi raia tufanye nini kama si kurisi.
   
Loading...