Tahadhri kuhusu unyanyapaa

Tumbo Chura

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2020
Posts
221
Reaction score
511
Naomba niwape angalizo kidogo baada ya kuona thread mbili tatu za kuhusu maambukizi ya ukimwi na waathirika kwa ujumla.
Nimeona baadhi wakitoa kauli za unyanyapaa ambazo kimsingi hazitujengi zaidi ya kuwavunja moyo waliopatwa na janga hili ambao wengi hawakukusudia.

Niwape mfano wa ndugu yangu ambae aliishi na shemeji yetu kinyumba kwa muda mrefu tu,sasa ikatokea siku ya siku anatafuta vyeti kwenye masanduku ambayo hawayatumii muda mrefu. Ghafla anakutana na dawa za kupunguza makali na vielelezo kuwa Shem ni muathirika kitambo.

Yaliyotokea yakawa yametokea ila kilichonifanya niwashirikishe ni kwamba uamuzi aliouchukua ni kwamba kwa kuwa yeye hakuzaliwa nao basi nae anaugawa,sasa mwanzo kwa sababu alipaniki kuhusu Shem kwa hiyo habari yake ilisambaa kama mnavyojua Wabongo tulivyobarikiwa umbea,sasa yeyote anaemnyanyapaa anahakikisha anatembea na mpenzi au ndugu yake yeyote kwa makusudi.

Sasa basi nilikua nawashauri kauli za kuwanyanyapaa sio sawa kwa sababu wapo walioathirika na wametulia na wenzi wao badala ya kufurahia kuwa kifo cha wengi ni harusi.

Ni hilo tu.
 
right, unyanyapaa si mzuri, ujue jf wengi wetu tumeifanya family hivo matatizo yetu mengi twayaleta huku ili tupate faraja.
 
Cha msingi ni kuwapa faraja, waathirika hawana tofauti na mtu ambaye hajaathirika na mtu anayemnyanyapaa muathirika anakuwa siyo muungwana maake maisha ni Yale Yale..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…