Tahadhari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tahadhari

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jidu, Aug 24, 2012.

 1. Jidu

  Jidu JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,167
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 180
  Kumekuwa na wimbi la uhalifu kwa kutumia simu hivi karibuni.leo hii nilipokea simu kwa mtu asiyejulikana na kuniambia kuna Bonus ya tsh 10,000 anataka kunitumia kwenye a/c yangu ya NMB, nakunitajia yupo kwenye tawi fulani la NMB,hivyo nifanye hima kwa kumpa namba ya a/c yangu.Akiendelea kuniaminisha kuwa ni mfanyakazi wa NMB na kuniambia hivi karibuni nilileta Fomu yangu ya uhakiki juu ya a/c yangu.Nilijua ni tapeli kwa kuwa kwenye zile fomu tunajaza a/c namba zetu iweje yeye ashindwe kujua a/c yangu?.nikaja gundua kuwa details zangu amaezitoa kwenye kampuni ya simu ambayo nimesajili namba yangu hivyo basi na waasa kuwa haya makampuni ya simu hayana siri juu ya wateja wake kwani imekuwa rahisi kwa hawa matepeli kujua jina la mtu na namba ya simu kiurahisi .Hivyo chukueni tahadhari nimenusurika leo kesho inaweza mliza mwingine usikubali kutoa namba yako ya a/c ama ya siri kwenye simu hata kama atakuambia yeye ni GAVANA wa bank!Namba iliyonipigia ni hii 0784469847
   
 2. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kuna majizi mengi sana kuwa makini
   
 3. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2012
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Bora ulivyo iweka namba yake humu.
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  matapeli wamezidi
   
 5. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Pole sana Mkuu. Hawa ni wezi wanatumia njia mbalimbali. Na kwa hakika hiyo simu itakuwa ni ya mtu mwingine. Kwa mfano kuna namna ambavyo wanaijua namba yako ya simu kutumia hata marafiki zako (ni mtandao mpana) then wana-disable namba yako na kuchonga kitambulisho chenye picha tofauti but jina ni la kwako wewe. Basi anaenda kibanda cha namba za simu anasema nimepoteza simu na line hivyo nataka kurudisha line yangu, akilulizwa kitambulisho anatoa na jina ni lako ila picha fake. Basi simu ikishakuwa hewani wanaitumia kwa uhalifu mwingi sana ikiwemo hata kupigia marafiki zako simu na kuwaambia watume hela au napifa toka kampuni ya simu fulani hivyo umeshinda mil kadhaa ili kupata labda tuma pesa au pia nipe namba ya a/c benki na ukiwapa cha moto umekipata. Ukiona simu card yako inakupa error au neno not recognised wahi haraka sana mtandao wa simu kurudisha namba vinginevyo utalia.

  Wengine wanaiba hadi simu za mawaziri unasikia mimi waziri naongea hasa na wakuu wa taasisi akiwaambia eti nipe hela mtoto amefukuzwa ada na nitarudisha au pia kupiga kwa marafiki. Ni wengi wamelizwa na wanaripoti polisi but nashangaa hawa polisi hawatangazii umma ila wanabaaki kutangazia yale ya uongo tu. KOVA upo?
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwita, hiyo namba tena unakuta ni ya mtu innocent kabisa ila wanakuwa wamei-hack. Soma post yangu hapo juu. Usishangae wewe siku moja unakuja kukamatwa na polisi kuwa umeiba kumbe ni majamaa wametumia namba yako kuiba.
   
 7. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Tz kama Nollywood siku hizi!!!!
   
Loading...