Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,305
Kuna taarifa kwamba nchi za New Zealand, indonesia,Brunei na nyingine jirani ya hizo, zimetahadharishwa juu ya Tsunami inayokaribia nchi hizo baada ya tetemeko la ardhi la kiwango cha 8.9 kuipiga Japan na kusababisha madhara makubwa.
Kuna unconfirmed report ya kuwepo kwa Tsunami, tunafatilia
Zaidi fuatilia: http://ptwc.weather.gov/ptwc/text.php?id=indian.TSUIOX.2012.04.11.0845
TMA nao watatoa tamkp soon, fuatilia: HATARI:Tsunami kufika pwani ya Tanzania saa moja leo | Fikra Pevu | Kisima cha busara!
Latest update inasema:
A SIGNIFICANT TSUNAMI WAS GENERATED BY THIS EARTHQUAKE. HOWEVER, SEA LEVEL READINGS NOW INDICATE THAT THE THREAT HAS DIMINISHED OR IS OVER FOR MOST AREAS. THEREFORE THE TSUNAMI WATCH ISSUED BY THIS CENTER IS NOW CANCELLED.
Kwa hiyo Kimbunga arudi tuu kutoka huko kilimani.
Fikra PevuTaarifa zilizotolewa jioni hii, zinaeleza kwamba tahadhari kuu sasa imeondolewa baada ya kutokea kwa tetemeko la baharini pwani ya Indonesia na hivyo kupunguza nguvu ya Tsunami katika eneo la pwani ya Hindi, iliyosababisha kizaazaa katika eneo hilo.
Hata hivyo, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na vyombo vya kimataifa vinaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya bahari, ufuatiliaji unaofanyika kwa saa 24 na kutatolewa taarifa za mara kwa mara itakapobidi.
Updates:
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) Dr Emmanuel Mpeta, amesema (19:20hrs EAT) athari za Tsunami kwa Tanzania sasa zimepungua sana na kwamba muda si mrefu atazungumza kwa kirefu kwenye TBC1, ambao walikosea kutangaza tahadhari sasa. Hata Waziri William Lukuvi ameshatumiwa taarifa sahihi za hali ilivyo kwa sasa. Hata hivyo, tahadhari bado ipo japo si kubwa kama ilivyokuwa mapema leo