Tahadhari: Wizi wa watoto Dar na Dodoma

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
20,090
46,367
Huu mchezo unataka kurudi Tena matukio haya ni Kama yalipoa ndani ya mwaka uliopita lakini 2019 kuelekea 2020 majambazi wameanza Tena kuteka Watoto.
mtu mmoja ananisimulia tukio lilitokea dodoma kwamba jamaa alivamia mida ya mchana ambapo hio nyumba Kuna watu wachache akataka kumwiba mtoto akawa anahangaika naye kuruka ukuta coz hio nyumba ilikuwa imefungwa geti akahangaika mpaka akakutwa mwisho akafanikiwa kukimbia.
pia dar kuna mtoto aliibwa tabata akapatikana bagamoyo akiwa analia asubuhi.kuna mwingine tena nimepewa stori aliibwa mitaa ya gongolamboto mpk Leo hii hajaonekana.matukio Ni mengi na visa vinazidi kuonyesha wanatumika kwenye mambo ya ushirikina.tuchukue tahadhari na tuwe waangalizi wa watoto wetu na wa majirani zetu. watu hawaaminigi siku hizi maisha magumu so watu wanajikuta wametumbukia kwenye waganga ambao wanawapa masharti ya kuua watoto au kupeleka viungo fulani vya mwili.
 
Back
Top Bottom