Tahadhari: Vifo vya mbwa hasa maeneo ya Dar es Salaam & Pwani

Bakulutu

JF-Expert Member
Nov 30, 2011
2,544
1,760
Kuna ugonjwa unapukutisha mbwa haswa, tumezika mbwa wengi sana na hasara kubwa kujaribu kuwakoa.

Sasa hivi kuna cases za mbwa kuugua ugonjwa wa Leptospirosis. Ugonjwa huu husababishwa na bacteria waitwao Leptospira canicola au Leptospira icterohaemorrhagiae. Ugonjwa huu ni zoonotic disease. Ugonjwa huu mara nyingi hutokea kipindi cha mvua kubwa kwa sababu bacteria hawa hupenda kuishi kwenye maji yaliyotuama.

Ugonjwa huu mara nyingi huwapata wale mbwa wa kisasa (exotic dogs) kama vile German shepherd, Rottweiler, Bulldog, Doberman Pinschers, Labrador, Dalmatian n.k. Ugonjwa huu pia huwapata ng'ombe, nguruwe na panya.


Ugonjwa huu hushambulia figo na ini. Mbwa aliyepata ugonjwa huu huonyesha dalili zifuatazo:- homa (40 - 41°C), kutochangamka, kukosa hamu ya kula, kutapika matapishi ya kawaida au damu, kuhisi maumivu ukimgusa sehemu za tumbo/tumbo kuwa gumu ukiligusa, ulimi kupoteza rangi yake na kuwa na michubuko, harufu mbaya mdomoni, kuharisha, kuwa na rangi ya manjano kwenye sehemu mbalimbali za mwili kama kwenye ulimi, fizi, macho, sehemu za chini za tumbo, vagina (jaundice), kunya kinyesi tepetepe cheusi kama lami (meleana).


Matibabu ya ugonjwa huu ni kama ifuatanyo:- Penstrep au OTC kwa siku 3 - 5, Fluid therapy, Vitamin B.


Kinga ya ugonjwa huu ni kuwatenga mbwa wagonjwa na wale wazima, usafi wa banda la mbwa, kudhibiti panya na kuwapatia mbwa CHANJO ya ugonjwa huu (DHLP)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom