Tahadhari Tume Teule ya Bunge.!

nrongalema

Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
48
Points
0

nrongalema

Member
Joined Apr 11, 2011
48 0
Naibu Spika ametangaza kuundwa kwa Tume(Kamati) Teule ya Bunge kuchunguza mchakato wa kurudishwa kwa Jairo kazini na kudhalilishwa kwa Waziri Mkuu pamoja na Bunge kulikofanywa na Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Luanjo.

Wana JF ninaomba tubainishe sifa za wajumbe wa hiyo kamati/tume maana ninahisi harufu ambayo siyo nzuri kama tahadhari haitachukuliwa...

ninapendekeza yafuatayo:

1. tume iwe na wajumbe makini.
2. tume iwe na wajumbe wasioshawishika.
3. tume isiwe na mafisadi.
4. tume isiwe na lengo la kulipiza kisasi.
5. tume isitoke nje ya hadidu za rejea.
6. tume itende haki kwa kila muhusika.
7. tume itupe matokeo yatakayotupeleka mbele na siyo yatakayotuchezesha mduara.
 

Forum statistics

Threads 1,353,874
Members 518,415
Posts 33,083,596
Top