Tahadhari; Tatizo la macho na matumizi ya simu

Tahadhari; Tatizo la macho na matumizi ya simu

MTAZAMO

Platinum Member
Joined
Feb 8, 2011
Posts
20,215
Reaction score
35,884
Wakuu,

Kama mnavyojua matumizi ya simu yamekuwa makubwa kwasababu ya kukua kwa huduma za mitandao na hivyo mambo mengi kufanyika kupitia simu za kiganjani.

Je tumewahi kupata taarifa za kiafya tunapaswa kutumia simu kwa kiwango gani kupunguza madhara mbalimbali na hasa macho?

Nashauri TCRA kupitia wizara ya afya waje na muongozo salama wa matumizi sahihi ya simu za kiganjani otherwise kuna kizazi kitapofuka kabla hata ya uzee tuanze kudeal na matokeo.

Nimeandika uzi huu baada ya kuwa inspired na hatua ya bingwa wa masumbwi duniani Anthony Joshua kuamua kupunguza matumizi ya simu za kiganjani ili aongeze uwezo wake kupitia macho kureact kwa haraka.

World class professional boxer kama AJ lazima amepata ushauri huu kutoka kwa timu ya madaktari. Kwanini sisi tusiangalie namna ya kupata taarifa sahihi pia kama wananchi?

Tuchukue tahadhari kabla ya kudeal na matokeo kama ilivyo ada yetu.

Screenshot_20190525-164817_Instagram.jpeg
 
Kabsaa, halaf mwingne nusu ya huo mda anatumia kuangalia nyuchi, unakuta mtu anaangalia simu mpk akiangusha udenda ndio anashtuka half ukiuliza anacho angalia? Kmb ni video ya gwajima au biriani
 
kbsaa, halaf mwingne nusu ya huo mda anatumia kuangalia nyuchi, unakuta mtu anaangalia simu mpk akiangusha udenda ndio anashtuka half ukiuliza anacho angalia? Kmb ni video ya gwajima au biriani
Kiukweli muda unaotumika kwenye simu inaogopesha sana. Bora tupate guardline ili kama unazidisha ujue na shimo lake.
 
Hahaha ...hasa nyie wazee wa first reply mna hatari sana
Mkuu macho lazima yafanye kazi,lakini pia lazima kuyapa virutubisho Mkuu kama karoti kwa wingi,mboga za majani na virutubisho vingine viiiingi.sio macho tuu hata figo,ini,meno,ubongo lazima vilishwe hivi viungo mkuu,unaweza kupunguza matumizi ya simu halfu huvipi virutubisho ni kazi bure.
 
Mkuu macho lazima yafanye kazi,lakini pia lazima kuyapa virutubisho Mkuu kama karoti kwa wingi,mboga za majani na virutubisho vingine viiiingi.sio macho tuu hata figo,ini,meno,ubongo lazima vilishwe hivi viungo mkuu,unaweza kupunguza matumizi ya simu halfu huvipi virutubisho ni kazi bure.
Asante kwa elimu mkuu. Ila kiwango cha matumizi ya simu zama hizi inabidi serikali ijiongeze.
 
Ni nchi inayojali watu wake kwa maneno ya jukwaani. Watu wanalipwa mishahara kwa kodi zetu watufanyie kazi, lakini wapo busy na yao. Wanangoja yatokee ndio wasimame mbele ya camera.
 
Back
Top Bottom