Tahadhari na wito kwa wana Simba wote

Nguvu moja

JF-Expert Member
Oct 20, 2017
3,371
2,712
TAHADHARI NA WITO KWA WANA SIMBA WOTE:

Kumekuwa na wimbi linaloendelea sasa mitandaoni la kutoa mambo yanayofanya taharuki au kuleta mijadala milngoni mwetu.
Hasa taarifa hizi:

1. Kocha msaidizi fulani
2. Wachezaji hawa wanaachwa
3. Manara kafukuzwa
4. Rufaa kwa mchezaji flani
5. Kocha hafai nk nk.

Lengo kuu za taarifa hizi ni kupenyeza mpasuko kati yetu na kuleta mingongano ili tusiwe wamoja katika wakati huu mgumu sana kwetu tuna mechi 3 kubwa sana kipindi hiki cha week 2 toka sasa nazo ni Al Ahly, Yanga na Azam.

Wito wangu tupuuze na tusipost chochote za uzushi kuhusu hayo mambo kwenye group zetu wakati wake utafika na kila kitu kitajulikana sio sasa.

Mawazo na akili zetu zote tuweke kwenye USHINDI Bila Umoja hatuwezi kuweka historia vizuri.
Hakuna Haja ya kutoana maneno wala kejeli miongoni mwetu maana hazitatunufaisha kipindi kipindi hiki zaidi ya kupata matokeo.

TUWE PAMOJA TUHUZUNIKE PAMOJA TUFURAHIE PAMOJA

IMG-20190210-WA0020.jpg

tapatalk_1549291271966.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
February 10, 2019
Dar es Salaam, Tanzania

Timu ya Al Ahly SC tayari imewasili jijini Dar es Salaam, Tanzania na kujitupa viwanjani kupasha pasha mwili kwa mazoezi mepesi kuelekea siku ya Jumanne ambapo itapambana na Simba SC katika mchezo wa pili baina yao ndani ya michuano ya klabu Mabingwa wa Africa CAF Champion league.


Source : Al Ahly SC
Video ikionesha mazoezi ya klabu hiyo kubwa barani Afrika ktk viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, Tanzania.
 
February 10, 2019
Dar es Salaam, Tanzania

Balozi wa Egypt nchini Tanzania alifika kushuhudia mazoezi ya timu ya Al Ahly jijini Dar es Salaam na kuwatia moyo wachezaji kuelekea mpambano wao na Simba SC ya Tanzania. Anategemea waamuzi watatekeleza kazi yao vizuri na pia mashabiki wa Yanga Young Africans kuendeleza utamaduni wao wakati watani zao wa jadi yaani Simba wakicheza na Al Ahly.

Baadaye jioni Mh. Mohamed Jaber Abu Al-Wafa Balozi wa Egypt nchini Tanzania aliwaalika viongozi wa bodi ya klabu ya Al Ahly kujumuika naye kwa chakula cha jioni na kuweka mikakati ya ushindi. Source : «مرتجي» يلبّي دعوة السفير المصري في تنزانيا على العشاء

Egypt's ambassador to Tanzania talks about Ahli's clash with Simba SC when he joined them at the Gymkhana Play Grounds in Dar es Salaam, Tanzania.
Source : Al Ahly SC
 


H
Hafla aliyoandaa Mh. Balozi wa Egypt Tanzania kwa viongozi walioandamana na timu ya Al Ahly kuja Tanzania ili kuwatia moyo na mshikamano viongozi na wachezaji wa timu ya Misri kuelekea pambano lao na Simba SC.
 
February 10, 2019
Dar es Salaam, Tanzania

Akiwa katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, Memba wa bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Al Ahly SC Bw. Khaled Murtaji akizungumzia matayarisho yao mazuri kuelekea mechi yao na Simba SC.

Kipa namba moja Mohammed Al-Shennawi wa Al Ahly yupo fiti baada ya kuwepo wasiwasi kufuatia kupata maumivu madogo katika mguu wake wa kulia mazoezini ktk viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam, hayo yamethibitishwa na uongozi wa klabu.


Khaled Murtaji, a member of Al Ahli's board of directors, talks about preparations for their CAf Champion League match against Simba SC in Dar es Salaam, the biggest commercial city in Tanzania on Tuesday the 12th of February 2019.
source : Al Ahly SC
 
hao wachezaji wazembe waendelee kukumbushwa kwamba pale siyo picnic, they either have to step up au waondoke. kina muzamiru, salamba nan wenzake wanachezea nafasi tu, useless kabisa
 
Back
Top Bottom