Masulupwete
JF-Expert Member
- Feb 15, 2012
- 2,366
- 2,438
Nadhani Serikali ingeliangalia hili suala la camps! Ni makundi ya wahuni hatari.
Nikiwa katika pilikapilika zangu za kipindi cha pasaka nilikutana na kituko kimoja kilichonishangaza na naona ni vema nikashea hapa. Nikiwa eneo la ilala bungoni DSM nilishuhudia trafiki akisimamisha gari aina Toyota coaster iliyokuwa ikitokea buguruni kuelekea mjini kwa ajili ya ukaguzi wa kawaida.
Katika hali ya mshangao mara baada ya gari kusimama kundi la abiria ambao wengi ni vijana wadogo pengine hawajazidi hata miaka 20 waliruka kupitia madirishani na kutokomea mitaa ya jirani. Trafiki alikagua gari na kukuta silaha za hatari zikiwemo mapanga, rungu, sime na vitu vingine vyenye ncha kali.
Kulikuwa na mazungumzo kuwa vijana hao ni kawaida yao kukodi gari wakidai wanaenda beach kuogelea lakini pindi wakifika huko hutumia hizo silaha kupora watu wanaowakuta huko. Vijana hawa wamejiunda kwenye makundi yao maarufu kama camps.
Kwa wapenzi wa picha mtanisamehe sikufanikiwa kupata picha mchina wangu aliisha chaji ningewawekea muone tunakoelekea
hivi watoto wa mbwa bado wapo mitaani?
hao jamaa wana 'barka' zote za kiserekali si ajabu hata hilo gari hawajakodi wao. nimeshuhudia kwenye shughuli zao utakuta diwani ndo mgeni rasmi!!
hivi watoto wa mbwa bado wapo mitaani?
Inasikitisha sana na jambo jingine mimi linanishangaza sana hivi kwa nini serekali inaruhusu mtu atembee na silaha kama kisu vijana wengi siku hizi utawakuta wamebeba visu wanaweka kiunoni wanafunika na nguo zao za juu kama shati au fulana'kuna siku asubuhi mapema nilikutana name jamaa kalewa sana kisha kiunoni kachomeka kisu tulikua wawili tu niliogopa sana siku nyingine nimepanda daladala kijana katika kujishikilia nikaona kachomeka kisu kiunoni nikajiuliza sana hivi visu wanavyobeba huwa vya nini. mi naomba mapolisi wawe wanawasachi vijana wengi wanapenda kutembea na silaha
Miji ya Tanzania inakua jamani, kwenye miji mikubwa gangs ni kawaida, sasa subirini hawa wapate waajiri wenye pesa na nguvu ndiyo mtachoka. Nunueni siraha mjiloinde, polisi hawawezi kukuhakikishia usalama.
Mimi huwa sikosi siraha napoenda mitaa hatarishi katika mida hatarishi, nyumbani mashine ipo imetulia, nakaribisha vibaka nina ham sana ya kuripua.
View attachment 153037