Uchaguzi 2020 Tahadhari muhimu kwa CHADEMA na ACT Wazalendo

SUASO

JF-Expert Member
Oct 19, 2017
770
1,188
Kuelekea uchaguzi wa tarehe 28 naomba Chadema na ACT Wazalendo mchukue tahadhari muhimu

1) Kuhusu mawakala wenu, wajiamini, wawe makini na matukio yote, wawe wenye uzalendo maana pesa nyingi zitamwagwa siku hiyo. Pia wawahi mapema sana kabla ya saa moja maana mbinu chafu zinapangwa kutumika mapema sana asubuhi!

Pia washirikiane wote yaani wakala wa chadema na ACT- Wazalendo wawe kitu kimoja, hii itasaidia sana kupunguza mianya ya wizi.

Pia wasikubali kutolewa ndani ya kituo husika kwa sababu yoyote Ile!

2) Viongozi wakubwa wa Chadema na ACT Wazalendo kote bara na visiwani wawe makini Sana, tena sana maana mawasiliano yao yanafatiliwa, hivyo ikiwezekana kutumia njia mbadala ktk mawasiliano aubkubadili kabisa namba za simu, hii njia inatumika na kitengo ili kuzima mawasiliano na kuweza kuthibiti haki ya kutoa matokeo kwa wagombea hasa urais na ubunge.

3) Kuna uwezekano wa kuzima internet siku hiyo na zinazofuata, je mmejipangaje kukabiliana na hili? Pia mawasiliano yenu yakafungiwa hivyo vigumu kuwasiliana na kutoa updates mbalimbali, mjipange na kuchukua tahadhari muhimu zote!

4) Ulinzi na usalama wa wagombea wote urais, ubunge na udiwani. Hapa kuweni makini sana maana mipango yao ni kuwathibiti chini ya Ulinzi pindi tu muda wa kupiga Kura unapoisha saa 10, fanyeni mikakati makini na mathubuti ili kuepuka hii mitego, kuwa chini ya Ulinzi , kuporwa simu na kunyimwa haki ya kuonana hii ndo mipango iliyopo jikoni!

5) Himizeni watu wasiende mbali na vituo vyao vya kupigia Kura, maana kura feki zitaingizwa hivyo uwepo wa watu utasaidia sana kufatilia vitendo viovu vyote!

Mwisho, nawaomba kuweni watu wa vitendo, tumechoka uovu, kama jino basi iwe jino kwa jino!

Haki, Usawa na Amani ndo msingi wa uchaguzi huru!

Chagua Lissu, chagua Chadema, chagua ACT Wazalendo, chagua Maalim Seif!
 
Unawaagaza Haya Wakati Weshashindwa uchaguzu Magu kaivuruga Kaskazini Hawaamini
 
Chadema acheni uoga, kipigo kipo pale pale
Waache wajitishe tuu mkuu😁😁😁😁
Siasa ni sayansi na sayansi ni namba. Tunawashukuru kwa kushiriki

IMG-20201022-WA0086.jpg
 
ujumbe wako tumeupokea na tunayafahamu hayo,tumejipanga vilivyo
Kila mgombea ubunge agakiki mfumo wa mawasiliano toka kila kituo kwenda kwenye kata na jimboni na taifani. Najua mawakala hawataruhusiwa kuwa na simu lakini tafuteni njia mvadala ya kuhakikisha mawasiliano yanakuwepo.

Agenda ya Nguvu ya uma iwe on place kwa sababu kuna kila dalili ya uhujumu. Andaeni umma. Ccm ni wachezaji, ni refa, washika vibendera, na makamisaa. Msiamini kabisa system.
 
Back
Top Bottom